Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIFAHAMU FURSA 10 ZA KILIMO ZISIZO HITAJI PESA KUWEKEZA.

Wengi wanaposikia biashara ama kuwekeza . Kitu cha kwanza wanasema inahitaji mtaji kiasi gani ??? Si kweli kwamba kila biashara inahitaji mtaji kufanya. Hapa unaanza kuwaza kama utani vile . Vipi nipate pesa bila kuwekeza pesa..???kwanza fikiri hili mpaka unaona sahani la wali mezani kuna mkulima Kyela alilima huo mpunga, ila lazima kuna kampuni ya mbegu ilimuuzia huyo mkulima izo mbegu na pembejeo . Bila kusahau kampuni ya usafirishaji iliofikisha mchele uliokobolewa baada ya mfanya biashara kuongeza thamani na kuhakikisha mchele unafika sokoni kwa wakati unaohitajika na mtumiaji . Huu ni mtiririko  wa matukio unao tokea kuanzia bidhaa ya kilimo inatoka shambani hadi inamfikia mtumiaji mezani yaani ( Agricultural Marketing). Humo katika mtiririko huo kuna fursa nyingi mno ambazo kazi yangu leo nikukufumbua macho na wewe uzione . Aya twende kazi mkuu

Matokeo yoyote ya biashara ni bidhaa ama huduma ( goods or services). Duniani kuna nchi ambazo uchumi wake hutegemea zaidi bidhaa( production economy) mfano Ujerumani,China,Brazili, ama Agentina . Lakini pia kuna nchi ambazo hutegemea huduma zaidi( service economy), kama Marekani, Ubelgiji ,Israeli,Uhispania na Ufaransa . Ni kweli uzalishaji wa bidhaa ( goods)yoyote unahitaji pesa ( production cost) tena katika kilimo uzalishaji wowote mkubwa unahitaji mtaji mkubwa mno. Habari njema katika hili ni kwamba uzalishaji ama utohaji wa huduma ( Agricultural services) aidha unahitaji mtaji mdogo sana wa fedha ama haiitaji mtaji kabisa . Kwenye makala iliopita tulijifunza kuwa mtaji sio lazima uwe pesa . Inaweza ikawa mawazo, ujuzi ,muda, uzoefu ama taarifa . Kama sijakuacha mpaka hapo jipigie makofi . Sema nimeshatoboa maisha . Leo tunaongelea ( Agricultural services opportunities)

Mwanzoni wakati tunaanza tumejaribu kugusia kidogo swala la " sahani la wali" tunaweza gawanya mchanganuo ule katika muktadha kadhaa yani shambani , usafirishaji, kuchakata , sokoni na ujuzi wa kufanya vyote ( Agricultural knowledge)
. Basi na fursa tutakazo pitia leo zitakuwa katika hizo sekta za mnyororo wa thamani ( Agricultural value chains nodes)

A. SHAMBANI

Eneo hili ndio eneo mama ambalo uzalishaji wa aina zote hufanyika . Tukisema shambani namaanisha eneo lakufugia samaki au mifugo na  eneo la kupanda mazao. Shuguli kubwa inayofanyika hapa ni uzalishaji . Jiulize tu kwa haraka ni huduma  ( service) gani zinahitajika hapa ili niweze kubadilisha uhitaji huu kuwa fursa ?

                                

1. MBEGU

Kwa Tanzania kuna makampuni makubwa ya mbegu kama SeedCo,Panar,Kibo Seed na Interchick ( viranga). Makampuni haya huzalisha na kuwauzia mbegu bora wakulima . Japo kuwa kuna nakampuni mengi ya mbegu ila kuna wakulima wengi zaidi ya nusu ambao hadi leo hawatumii mbegu za dukani sio kwa sababu hawana pesa za kununua ila ni kwakuwa hawana aidha taarifa juu ya mbegu ama walipo hapafikiki kiurahisi . Mtu anaweza sema sasa apa fursa iko wapi mzee??  Fursa hapa nikuwataftia viwanda vya mbegu wakulima ambao wapo tayari kununua mbegu zao . Kama wakulima watakuwa wengi  kiasi cha kushawishi kiwanda kupeleka moja kwa moja kwa wakulima wewe utakuwa kama mtu wa mauzo na kiwanda kitauza kwa bei ya kiwandani kwa wakulima wako na wewe utauza kwa bei ya sokoni baada ya kutoa gharama za usafirishaji.  Hapa atakae peleka mbegu ni kiwanda ama wasambazi wakubwa . Wewe unachohitaji kufanya ni kuongea na wakulima kuwaelimisha na kuwashawishi . Hapa mtaji wako ni taarifa sahihi, wakati sahihi na kwa mtu sahihi

                                                                   

2. SHAMBA
Eneo hili ni eneo linalotumika kwa uzalishaji . Kutokana na ongezeko la taarifa, uhitaji wa chakula na ufahamu wa watu . Kuna ongezeko kubwa la maeneo ya watu kutaka kuwekeza katika kilimo. Idadi kubwa ya watu hawa huwa hawana taarifa kabisa kuhusu wapi walime , walime nini . Ama wapi wafuge na wafuge nini. Wamiliki wengi wa mashamba huwa ni makampuni, taasisi, vikundi, serikali ama watu binafsi.  Apo unawaza sawa tunajua haya yote fursa iko wapi apo ? Kama utatumia muda wako kujua wapi unaweza pata maeneo mazuri ya kilimo ama mashamba unaweza waunganisha wahitaji wa mashamba hayo na wamiliki kisha wewe ukapana na mmiliki na muhitaji na ukapata pesa kama mtu  wakatikati apa unakuwa umetoa  huduma( Agricultural land services). Mtaji mkubwa hapa unaohitaji ni muda na taarifa na kuwa na watu sahihi yani ( connection).

                                                          

3. MBOLEA NA VIWATILIFU
Kwa  bahati mbaya asilimia kubwa ya watu wengi wanaofanya Kilimo katika nchi zetu za Kusini mwa Jangwa la Sahara sio wataalamu wa kilimo kwa maana ya ( formal Agricultural knowledge)
Hili ni tatizo kubwa kwakuwa wengi hawajui watumie dawa ama mbolea  gani, lini  ama kipindi gani. Hapa wewe unachohitaji ni kwanza kuwapa elimu wakulima kisha kuwasadia kukadiria uhitaji wao wa mbegu na madawa. Kisha hapo utaongea sasa na wazalishaji baada ya kuwa na uwakika na soko . Wao watawasambazia kwa bei ya jumla alafu wewe utakuwauzia kwa bei ya soko . Hakuna mgavi ( distributor) yoyote atakae jihakikishia soko la gunia 1000 za mbolea akatae kupeleka huko .

                                                

4. TEKNOLOJIA
Kwa sababu ya ukuaji wa uhitaji unaosababishwa na ongezeko la watu . Teknolojia ya kilimo imesaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji. Teknolojia hizi ni kama utengenezaji wa ( green house) , upimaji wa udongo ama mifumo ya umwagiliaji. Katika ongezeko la utumiaji wa Teknolojia ya kilimo bado kuna wakulima wengi hawafamu namna ama wapi pa kupata Teknolojia hizi . Kumbe unachohitaji wewe apo ni kutafuta uhitaji alafu kuunganisha muhitaji na mtoa huduma . Labda nikupe mfano ili unielewe vizuri . Unaweza tafuta mkulima anae taka kufungiwa mfumo wa umwagiliaji wa matone ( drip irrigation system) ukamwbia tunaweza kukufungia mfumo huu kwa shilingi milion  3 . Alafu ukaenda katika kampuni ya  Teknolojia hii ukawambia nataka mje mtufungie  mfumo wa umwagiliaji shambani kwetu kwa shilingi milioni 2 . Baada ya wote hawa kukubali. Unasaini mkataba na mtoa huduma alafu unasaini mkataba na mkulima . Biashara inafanyika. Unaweza fanya hivi kwenye huduma zingine kama kupima udongo nakadhalika . Hapa kazi yako kubwa ni watafuta wanaotoa huduma hizi . Ila uhitaji ni mkubwa mno na unazidi kuongezeka . Changamka sasa uskae kinyonge ndugu yangu.

                                                               

B. USAFIRISHAJI

5. Moja ya njia ya kuongeza thamani katika mazao ya kilimo ni kusafirisha . Yaani kutoa sehemu ya uzalishaji mkubwa na uhitaji mdogo ( low demand and surplus  unit) kupeleka sehemu yenye uhitaji mkubwa ( high demand deficit unit) . Katika nchi yetu sekta hii imekuwa na changamoto kubwa hasa kipindi cha msimu wa  mavuno. Wengi huwategemea madali ili kupata magari . Watu hawa kwa muda mwingine wamekuwa wakitoza wafanya biashara pesa kubwa mno kuliko uhalisia wakati mwingine . Mfano mwezi wa sita hadi wa tisa kutoa kilo moja mfano ya mahindi Mbeya hadi Dar es salaam ni Tsh. 120 kwa kilo wakati mwezi wa kumi hadi watano ni Tsh. 80 kwa kilo . Wapo watu wengi mizigo yao mingi imepotea  ama kuharibika sababu ya kukosa watu waamininifu wa usafirishaji.  Nadhani mpaka hapa umeshaona fursa . Kwanza unahitaji kufahamu wamiliki ama makampuni ya usafirishaji ( apa ask Mr. Google) ukishapata hili unaweza tumia hao hao madalali kupata wateja wanaohitaji usafirishaji kisha hapo utengeneze wateja wako . Kwa kila gari utakalo mtafutia mteja unaweza kupata kati ya elfu hamsini hadi laki tatu. Mfano mzuri tuu kwa mkoa wa Sumbawanga na Songwe hiki kipindi cha mavuno kuna uhitaji wa zaidi ya malori zaidi ya 50 kwa siku moja . Huu ni mfano tuu wa mikoa hio . Vipi mikoa mingine .  Embu fanya uamke usingizini . Tazama fursa hizi. 

KUONGEZA THAMANI

Kama bado haujasahau mfano wetu wa kwanza wa wali upo juu ya meza. Mkulima analima mpunga ila mezani unafika wali .Manake hapo kuna kuongeza thamani  kuliko ongezaka. Sasa tupitie fursa zinazopatikana hapa
                                    

6.KUCHAKATA NA VIFUNGASHIO VYA BIDHAA YA KILIMO

Bado wakulima ama wafabiashara wengi baada ya kuchakata mazao yao mfano baada ya kukoboa mpunga wanauza vile vile tu kwenye magunia ambayo wakati mwingine yanakuwa machafu na vifungashio duni visivyo na ubora na mvuto kwa mteja ( poor convince)Kuna watu wa hali fulani ya maisha hawawezi tumia bidhaa hizi . Fursa iliyopo hapa ni katika kufanya ufungashaji( package and branding) hapa inahitaji kumshawishi mkulima ama mfanya biashara kubadili mfumo wa kuhifadhi. Mfano unaweza mtengenezea logo ili atambulike alafu kisha unaweza mshauri kutumia mfano kwa mchele ama unga ( water proof sacs) . Sasa fursa inakuaje . Apa huitaji kujua kutengeneza logo hapana . Tafuta mtu anae jua kisha ongea nae bei alafu nenda kwa mkulima ongea nae bei . Tafuta kampuni za kuprinti magunia mkulima atakupa pesa ya kununua magunia yasio na chapa( plain) alafu wewe mpe bei ya ( branded sac) alafu msaidie kufunga mfano badala ya kushona kwa mkono ashone kwa mashine . Hapa wamashine utamlipa wewe alafu wewe utalipwa na mkulima ama mfanya biashara . Kama umenipata hapa tumezungumzia fursa zaidi ya mbili.

                                           

7.GHALA
Katika hili kuna swala la maghala ya chakula . Skuizi vijiji vingi vina maghala ya chakula . Kwanza unahitaji kutafuta ghala na kujua thamani ya kulikodi .Mfano thamani ya kulikodi ni milion 12 kwa mwaka yaani milion 1 kwa mwezi . Na kama linaweza weka gunia 15,000 . Kwanza msimu ukikaribia nenda uongee na wakulima juu ya lengo lako la kuwahifadhia mazao kwa msimu huo . Kama unaweza  kuwachaji 1500 kwa gunia kwa mwaka mzima yaani ( tsh 125 kwa mwezi kwa gunia). Maanake utapata Mauzo ya zaidi ya milioni 20. Lakini vitu sio rahisi kiasi hiki kama  ile biashara ya matikiti au ya kuchoma mahindi ama " ponzi scheme" . Biashara haiwezi kuwa imenyooka hivyo we umekuwa nani . Kwanza hakikisha umepata wakulima wa kuhifadhi sababu wakulima wengi huwa wanauza moja kwa moja . Alafu pesa ya kwanza ya kulipia ghala utaipata kwa wakulima ambao wako tayari kuhifadhi . Ila katika hili unaweza wapangishia hawa wakusanyaji wadogo wadogo . Biashara hii ni rahisi sana kuifanya maeneo wanayolima mpunga maana  ndio wengi wao wanaweka  na sehemu za mahindi mengi kama songea  , songwe au sumbawanga.  Lakini narudia kukumbusha sio rahisi kiasi hicho . Inahitaji mtu  makini na mwenye kujituma sana

D. SOKONI
Wataalamu  wa kilimo biashara wanakuambia uzalishaji unaanzia sokoni na  sio shambani ( production starts at the market) . Kwa maana nyingine ni soko ndilo linaamua uzalishe nini, lini , wapi na kwa kiwango gani . Soko ndilo linaongoza uzalishaji . Hapa ndipo kuna fursa kubwa zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo . Tujaribu kuangalia fursa chache tu.


                        
8. KUUNGANISHA WAKULIMA NA MASOKO.

Ukweli ni  kwamba wakulima wengi huwa wanalima mazao yao na hawajui amuuzie nani . Kama ukiweza kuwataftia wakulima wateja wa kununua mazao yao basi unaweza kujiingizia kipato kikubwa . Lakini pia kuna makampuni 90 makubwa ama wagavi yanayotafuta mazao . Ukiwataftia hawa masoko basi unauwezo mkubwa wa kujiingizia kipato  kwakua wahitaji wengi  wa mazao wana mitaji na wana uwezo wa kuyafata yalipo . Alafu katika hili kuna mazao zaidi ya 100 unayoweza kuyafanya kuanzia nafaka , mboga mboga, matunda ,Miche ama mifugo. Changamoto kubwa ya fursa hii ni mabadiloko ya bei. Bei za bidhaa za kilimo zinabadilika kila leo kila mara ( volatility ) sasa ili uweze kujipatia kipato kupitia fursa hii ni lazima uwe  na ufatiliaji wa hali ya juu sana tena wakila wakati kuhusu hali ya masoko . Kutokana na madiliko ya mifumo ya serikali unahitaji mtaji mkubwa wa watu sahihi wenye taarifa sahihi ili kufanikisha bishara katika nyanja hii.

Katika fursa ya kuunganisha wakulima na masoko ipo fursa nyingine mipakani yani kama Namanga Arusha, Mtukura Kagera, Manyovu Kigoma ama Tarakea Kilimanjaro.  Katika sehemu hizi kuna wakulima  huitaji kusafirisha mizigo yao ama kutafutiwa wateja wa mazao yao . Unaweza toa huduma ya kuwasidia kwa kuwaunganisha na ma ajenti wavushaji ama wateja wanunuzi na wewe ukalipwa ( marketing fee) . Katika sehemu hizi masoko ni makubwa na mazao ni mengi mno unaoweza kuyafanyia kazi . Jaribu uwe na ufatiliaji tu , utanishukuru badae.

                          

9. MTANDAO

Katika zama tunazoishi ( information age) kuna ukuaji mkubwa wa usaambaaji wa taarifa kwa njia ya mtandao. Kila leo watumiaji wa mtandao wanazidi kuongezeka . Mtandaoni inakuwa ni sehemu rahisi sana kupata  wateja mbalimbali.  Fursa hii unaweza itumia kwa kutumia kutangaza fursa zote tulizojadili hapo juu . Mtandaoni unaweza tangaza bidhaa za kilimo za watu wengine ama bidhaa zozote alafu ukaweka na bei ( marketing fee) yako ili uweze kupata faida. Hii njia skuizi  wengi hutumia kwenye nguo na simu. Sasa unaweza tumia kwenye bidhaa za kilimo . Ugumu wake ni kwamba tofauti na nguo ama simu zenye bei isio badilika badilika .Bidhaa za kilimo zina badilika mara kwa mara . Hivyo unahitaji kuwa mfailiaji mkubwa mno.


                 

E. ELIMU

Kilimo biashara ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine . Kuitoa  taaluma hii kwa watu wengine ni fursa 
10. ELIMU NA USHAURI WA KILIMO.
Kutokana na uhitaji wa ulasimishwaji wa biashara nyingi za kilimo taasisi fedha ama benki haziwezi kufadhili biashara ya kilimo ambayo haijapitiwa na mtaalamu wa kilimo kuandika vitu kama " Agricultural busness plan " ama " designing Agricultural business systems " inahitaji mtaalamu . Katika kutoa huduma hizi za ushauri (Agricultural consultation) unaweza kujiingizia kipato. Lakini fursa hii inahitaji ujuzi . Ujuzi huu sio lazima uwe muhitumu wa elimu ya juu kwenye kilimo unachohitaji ni kujifunza tuu na kuweza kutumia fursa husika.

Bila shaka umejifunza  kitu . Usisite kutoa maoni yako  ili tuendelee kujadili mada hii na nyingine  mbalimbali kuhusu kilimo , uchumi na biashara.

Tunashukuru sana kupitia makala hii. Ubarikiwe sana .

Erick Muhini ( Agro Economist)

Wasiliana nasi kupitia:

+255744207795

ottomanerick@gmail.com

BONYEZA HAPA  kuwasilia nami whatsapp

Post a Comment

7 Comments

  1. Replies
    1. That's s great brother . Share it with friends as well

      Delete
  2. woow very fantastic ,nimeshare makala hii ubarikiwe uliyeandika

    ReplyDelete
  3. great tuna kitu kikubwa cha kujifunza hapa

    ReplyDelete
  4. Sisi ni wadau wa kilimo ,Tunatamani kuunganisha mawazo pamoja ,mnapatikana wapi?

    ReplyDelete