Biashara ni mfumo wa maisha wanaotumia watu wengi kujiingizia kipato. Sio kila mfanya biashara ni mjasiriamali lakini kila mjasiriamali ni mfanya biashara. Kama zilivyo sekta nyingine nyingi sekta ya biashara ni sekta yenye utamaduni,sheria na mifumo inayoiongoza ili iweze kutendeka. Biashara zimeanza kufanyika miaka mingi sana nyuma .Mfano waarabu walianza kuja pwani ya Afrika Mashariki kabla ya Karne ya pili kabla ya Kristo. Biashara ili iweze kuleta mafanikio inamuhitaji muhisika awe na namna fulani ya kufikiri na mtindo fulani wa maisha . Kuna mambo kadhaa yanayo husu biashara ambayo huwezi kufundishwa na taasisi zetu za elimu. Hii inatokana na mifumo mingi ya elimu iliopo kuwaanda watu kuwa waajiriwa na sio waajiri . Swala hili lipo hadi katika taasisi za elimu ya juu zinazofundisha uchumi,biashara ama ujasiriamali.
Ufutao ni ujuzi ambao ili uwe mfanyabiashara mwenye mafanikio lazima uwe nao na huwezi fundishwa ujuzi huu katika taasisi zetu za shule ziliozopo.
1. UBUNIFU ( CREATIVITY)
Ubunifu ni hali ya kutengeneza kitu kipya( creative imagination)ama kuboresha kilichokuwepo ( synthetic imagination) kwa namna ambayo haikuwepo mwanzo. Ni kweli ili uweze kuwa mbunifu ni lazima uwe na ujuzi fulani kabla utakao kufanya ama kukusaidia kuanza ubunifu huu. Ujuzi huu unaweza pata shuleni ama mtaani kutokana na mfumo wa maisha ulioupitia. Mazingira yoyote ya bishara ni yakubadilika badika kulinga na vitu mbalimbali kama tabia za watumiaji ( consumer dynamics), mabadiliko ya mifumo ya kiserikali, mfumuko wa bei ,ushindani na changamoto mbalimbali . Kutengeneza biashara itakayo simama na kukupa faida ya kudumu unahitaji ubunifu wa hali ya juu sana . Ubunifu huu hauuhitaji mara moja pindi unapoanzisha biashara ila unauhitaji kila siku, kila saa na kila sekunde. Hakuna mahali shuleni utafundishwa ubunifu . Unahitaji kujifundisha mwenyewe aidha kwa kusikiliza maoni ya watu ama kutumia ujuzi wa myuma na kubuni mbinu mpya ili kuendelea kusimama katika biashara yako. Hakuna biashara yoyote duniani ambayo huwa inakuwa imenyoka moja kwa moja . Hata makampuni makubwa kama Ferrari, Lambhogini,KFC yameshawahi kufilisika na yakainuka. Ni ubunifu ndio utakufanya ubuni mbinu mpya ya kutatua matatizo amabayo nilazima ukutane nayo katika biashara. Kwakua biashara yoyote huanzia sokoni basi ubunifu wenye tija utaanza kwa kujifunza ni nini wateja wako wanahitaji na wengine wanafanyaje kutimiza mahitaji na je ? Unawezaje kujitofautisha na wengine ili kupata wateja wapya na kuendelea kuwatunza waliopo ? Ukiweza kuwa mbunifu kiasi cha kubadilika kulingana na mahitaji ya wateja basi ni rahisi kutengeneza biashara yenye tija na itakayo weza kudumu kwa miaka mingi .

2. NIDHAMU YA FEDHA (FINANCIAL DESCPLINE )
Nidhamu ya fedha ni mfumo wa mipango kuhusu njia za mapato na namna ya kupanga matumizi. Watalaamu wa mambo ya fedha wanasema tajiri hutumia kilichobaki baada ya kuwekeza wakati maskini huwekeza kilichobaki baada ya kutumia . Nidhamu ya fedha ndio njia pekee itakayo fanya biashara yako isimame . Tunaweza kutambua nidhamu ya mtu ya fedha kwenye mambo anayopenda kutumia fedha yake ( preference in consumption) . Watu wengi wakipata mshahara huishia kununua matumizi hadi yasio yalazima na wengine huingia kwenye madeni jioni kwa kuwa na matumizi kuliko kipato ama kutaka kuishi maisha ya ghali kuliko uwezo wao.
Nidhamu ya fedha haifundishwi shuleni ila huja kwa mtu binafsi kuanza kujitambua yeye mwenywe .
Nidhamu ya fedha ni hali ya kujitambua hali yako kiuchumi , Namna ya kutengeneza mipango ya kuongeza kipato chako, kuzalisha kipato chako na kuanza kuwekeza kwenye vitu vinavyo ongeza kipato chako na sio kukipunguza ( asset first then liabilities).
Kama unampango wa kuwa mfanyabiashara ama una lengo la kukuza biashara ni lazima ujifunze nidhamu ya fedha na ubadili kabisa mfumo wa maisha wa kuhakikisha mipango na kipato chako kinaendana na matumizi na unapata kiasi hata kama ni kidogo cha kuwekeza. Hili litahitaji pia ujuzi na ufanisi katika uwekezaji huo.
Bila kuwa na nidhamu ya fedha haiwezekani kabisa kuweza kufanikiwa katika bishara yoyote . Utaanza biashara ila itakufa tuu bila kipingamizi.
3. UTULIVU WA KIHISIA ( EMOTIONAL STABILITY)
Hii ni hali ya kuweza kumudu kutunza hisia zako pindi ukiwa katika misukosuko( stress) . Uwezo huu ni msingi sana kwa mfanya biashara yoyote na kwa bahati mbaya shule haiwezi kukufundisha kuwa emotional stable. Mazingira ya biashara ni mazingira yenye mkazo ( stess) wa hali ya juu na hii inatokea kila siku kila leo . Kama ni kampuni kuna mkazo toka kwa waajiriwa, wawekezaji , taasisi za fedha, sokoni na hali nzima ya biashara. Ukiwa katika biashara unahitaji kufanya maamuzi kila mara , ili ufanye maamuzi unahitaji kuwa na akili iliotulia . Lakini biashara zinahusisha kupoteza ama kupata hasara je utawezaje kuvumilia hasara hio na kuendelea kuwa sawa kihisia na kufanya kazi na moyo ule ule .
Somo gumu zaidi katika biashara ni kuweza kujitenganisha hisia zako na pesa . Hii inamaanisha kama umepata faida ama umepata hasara hali ( mood) inabaki vile vile na matumizi yako hayabadilishwi na faida unayopata ama hasara . Ukiweza fikia halii hii kibiashara mafanikio ni swala tu la muda . Ila hali hii inapatikana ama inafundishika tu baada ya kupata faida nyingi ama hasara nyingi hadi kuzoea . Huwezi jifunza hili kwa kusoma vitabu . Mtu ambae amejitenganisha kihisia na feddha ni mtu ambae hajiwazii yeye mwenyewe ila huwafikilia wengine na matatizo yao. Watu waliofanikiwa wote wana sifa hii ya kuleta suluhu ( solutions) kwa matatizo ya watu wengine . Ukiangalia maisha ya watu wengi maskini ambao hawajafanikiwa ni watu ambao wanajifikiria wao wenyewe na wanaubinafsi wa hali ya juu. Kwakuwa hawawezi kutatua matatizo ya watu wengine basi ata kipato Chao kitakuwa kidogo tuu . Jifunze kuongoza vyema hisia zako ili uweze kuwa na matokeo chanya katika maisha yako na katika ulimwengu wa biashara

4.UWEZO WA KUUNGANA ( ABILITY TO CONNECT)
Uwezo wa kuungana ni hali ya mtu kuweza kuingia kwa urahisi kwenye maisha ya mtu mmoja ama mwingine . Uwezo huu huusisha namna ya kuongea na mtu , kutambua kiurahisi mtu mwingine ni wa namna gani na anahitaji nini na kumfanya mtu mwingine ajisikie huru ama salama anapokuwa na wewe. Hii ni sifa kubwa ya mfanya biashara aliefanikiwa na kwa bahati mbaya ni kazi sana kujifunza hili shuleni . Umuhimu wa sifa hii ni upi?
Ukiwa na uwezo mkubwa wakuungana na watu wengine itakusaidia sana kupata taarifa sahihi kuhusu biashara ipi nisahihi na ifanyike lini na wapi, kujua ki urahisi wateja wako wanaitaji nini hivyo itakuwa rahisi sana kutimiza malengo ya mteja wako. Pia uwezo huu utasaidia kuwapa motisha ama kuwaelekeza watendaji wenzako katika biashara na kuifanya biashara yako iwe yenye tija. Na rahisi kusimama hata kama itapitia kipindi cha kuanguka. Watalamu wa mambo ya masoko wanasema " people buy from emotion not from logic" yaani watu hununua bidhaa toka kwenye hisia na si uhalisia. Kumbe ukiweza kuungana na watu na kuteka hisia zao katika biashara yako una uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa katika biashara yako . Mfano halisi ni kama kampuni ya "Apple" ya simu aina ya" iPhone " ukweli ni kwamba kuna simu aina ya "Samsung " zenye ghalama kubwa marabili kuliko iPhone ya bei kubwa lakini watu hutumia aina hii ya simu kuonyesha uwezo wao mkubwa wa kifedha. Hii ni kwa sababu bidhaa hii imefanikiwa kuteka hisia za wateja kwa kuungana nao .Ukiweza kukuza uwezo wako wa kuungana na watu basi ni rahisi kukuza biashara yako na kuweza kufanikiwa katika sekta ya biashara

5. HALI YA KUTOKATA TAMAA ( PERSEVERANCE)
Hii ni hali ya kuendelea kufanya kitu kwa kasi ile ile hata kama viashiria vinaonyesha hakuna matokeo chanya. Ukweli ni kwamba biashara sio kitu rahisi . Takwimu zinaonyesha 90% ya biashara hufa ndani ya miaka mitatu ya kwanza ya kuanzishwa. Na 90% ya hizo zilizo baki ni 10% tuu huwa zinakuwa hai ndani ya miaka 10 . Hiii inamaanisha ni karibu asilimia kati ya 5 hadi 10 za bishara ndio hufanikiwa .
Katika maisha ya biashara misuko suko ni mingi kuna kuanguka mara nyingi kuna kugombana mara nyingi , kuna kuchekwa mara nyingi, kuna kusalitiwa na kutukanwa mara nyingi na pengine na watu ulio waaminini. Muandishi wa kitabu cha "The Success principle" Jack Canfield. Alisema " The only way to succeed is to take 100% responsibility for yourself" . Ili uweze kupata mafanikio katika biashara kuna ulazima wa njia nyingine kuzipita peke ako. Lazima uweze kupambana na kuinuka kila unaporudishwa nyuma . Ukifanikiwa kuweza hili basi mafanikio yako katika bishara ni swala la muda.
Haya ni baadhi ya mambo machache tu yamuhimu ila yapo mengine mengine mengi ambayo ili kufanikiwa katika bishara mtu anaitaji kujifunza.

Tunashukuru kupitia makala hii. Ubarikiwe sana
Wasilina nasi kupitia
+255744207795
Erick Muhini ( Agro Economist)
0 Comments