KWA NINI DOLA INASHUKA?
Kama utakuwa mfuatiliaji wa namna dola ya marekani inavyokwenda
utagundua kuwa dola imeshuka kwa kasi ukilinganisha na mwaka jana.
Kumekuwa na maswali mengi "Je uchumi wetu umeshuka?, Uchumi
wetu umepanda?, Je fedha yetu imeanguka au imeimarika?, Kuna faida yoyote
kibiashara au hasara?,
Je dola ikishuka kuna athari yoyote kwenye uchumi wetu?, Je
serikali inaweza kuratibu kupanda na kushuka kwa dola?,
Kwanza kwanini ishuke sasa hivi na sio mwaka jana?, Vipi
itaendelea kushuka tena ama itapanda?".
Maswali kama haya na mengine mengi watu kadha wa kadha
wamekuwa wakiuliza.
Kabla hatujaanza kuwajibu nadhani turudi nyuma kidogo.
UTANGULIZI.
Kama tulivyojifunza katika makala za nyuma kuhusu fedha. Ni
kipindi cha mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia mwaka 1944. Nchi 44 zilikaa (
Bretton Woods Agreement) na kukubaliana dola ya marekani itumike kama pesa ya
biashara kimataifa na ndio mwanzo wa kuanzishwa benki ya dunia na shirika la
fedha duniani( World bank and International Monitary Fund).Kuanzia hapo, basi
dola ya Marekani ( usd) ilianza kutumika kama fedha ya kibiashara ya dunia (
world trade currency) na ikapalekea benki kuu za nchi tofauti tofauti kuanza
kuhifadhi dola ( world reserve currency) ili ziweze kuitumia kuuza na kununua
bidhaa kwa mfumo wa kibenki wa kimaghalibi yani ( Swift sytem) .
Kulingana na uhitaji huu wa dola basi fedha hii ilikuwa kama
bihaa zigine. Moja kati ya sheria kuu ya uchumi , inasema kwamba kama bidhaa
ikiwa nyingi na uhitaji ni mchache basi thamani ya ile bidhaa inashuka na kama
bidhaa ikiwa chache na uhitaji mkubwa thamani ya ile bidhaa inapanda ( demand
and supply law).
Kumbe sababu kubwa inayofanya bidhaa ( dola ) ipande ama
kushuka ni uhitaji wake ( demand)
ukilinganisha na upatikanaji wake ( supply). Kwakua uthamani wa fedha hupimwa
kwa kulinganishwa na dola. Kumbe dola ikipanda ukilinganisha na fedha ya nchi
husika basi tunasema ile fedha imepungua thamani ukilinganisha na dola. Hali
kadhalika dola ikishuka ( kama ilivotokea sasa) ukilinganisha na fedha ya
Tanzania basi tunasema fedha ya Tanzania imepanda thamani kulinganisha na dola
ya Marekani.
Baada ya kupata utangulizi basi twende pamoja kwenye
uhalisia na ukweli hasa wa mambo.
KWANINI DOLA IMESHUKA THAMANI ?
Ili tuweze kulijibu swali hili kwanza inabidi tuwe na taswira
mbili kwanza ni taswira ya kidunia pili taswira ya nchini kwetu Tanzania.
Tukianza na kidunia, Katika utangulizi tulisema dola ni kama
bidhaa ( financial instrument), Kuna namna ambavyo mathalani hisa hupanda ama kushuka thamani kwasababu wawekezaji
wamepoteza imani ,ama imani imeongezeka kwenye hisa husika. Hii kitaalamu
huitwa investors confidence. Kuna sababu kadhaa
kidunia ambazo zimepelekea dola kushuka thamani .
1. Kupungua kwa imani ya dola kwa wawekezaji duniani
A) sera na deplomasia ya Marekani ,
Mfano Marekani ilizuia fedha za Urusi zaidi ya dola billioni
800 kwa sababu ya uvamizi Ukraini. Hii ilikuwa kinyume na sheria za fedha za
kimataifa. Hivyo nchi nyingine zinaona Marekani inaweza kufanya hivyo kwa nchi yoyote inayopingana nae kisera,
hasa kwa kuiwekea nchi husiks vikwazo
mfano ni Irani,bUrusi, Venezuela na Zimbambwe( weponizing of the currency).Ili
kuidumaza kiuchumi
B) Uchaguzi wa Marekani
Baada ya raisi mteule Donald Trump kushinda Uchaguzi wa Marekani. Kumekuwa
na matamshi ya kuongeza kodi ya 100% kwa magari ya umeme ( Electric Vehicles) kutoka
China ama kodi 10% kwa bidhaa kutoka nchi
zote duniani. Jambo hili linafanya nchi nyingine zipunguze imani na dola
ya Marekani.
Hizi sababu zinapelekea uhitaji wa dola upungue. Ukipungua
dola inakuwa nyingi kwenye mzunguko na hii inapelekea ishuke thamani.
2.Mabadiliko ya Uchumi wa Dunia ( Ukuwaji wa nchi za BRICS+)
Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia biashara zilifanyika kwa
dola kwa zaidi ya 83%. Lakini kutokana na ukuaji wa Uchumi wa China na mataifa
mengine, biashra nyingi sasa zinafanyika
kwa pesa ya China, India, Urusi, Japani na nchi nyingine.
Nchi za Brics+ hufanya baadhi ya biashara kwa kutumia pesa
za nchi husika na ziko kweye mpango wa kuwa na fedha yake. Hii pia inapunguza
uhitaji wa dola, jambo linalofanya dola
iwe nyingi kwenye mzunguko na kuifanya
izidi kushuka thamani.
3)Mazingira ya kiuchumi kidunia
Uchumi wa Dunia unategemeana( inter linked) baina ya nchi
moja na nyingine.Hapa ntakupa mfano mdogo. Nchi ya Japani ndio nchi inayoongoza
kwa watu kutunza fedha ( world no. 1 savers) na
wawekezaji wengi wa Kimarekani wamekuwa wakikopa fedha benki za Japani
kwakua riba ni ndogo na kuwekeza Marekani. Hivyo wawekezaji huuza yeni ya Japani
na kununua dola . Miezi kadhaa nyuma kutokana na matatizo ya kiuchumi, Benki
kuu ya Japani iliamua kuongeza riba(
interest rate). Hii ilipelekea wawekezaji wengi wa Marekani kuuza hisa zao ili
wanunue pesa ya Japani kurudisha mikopo ( market panic) halii hii inaongeza
dola kwenye mzunguko na kuifanya ishuke thamani zaidi.
Hizi ni baadhi tu ya sababu za kidunia zinazopelekea Dola
kushuka thamani.
KWANINI SASA DOLA INASHUKA THAMANI NCHINI
TANZANIA?
Kushuka kwa dola nchini haiwezi kuwa ni matokeo ya kushuka kwa dola kidunia peke yake, kwa sababu. Tukiangalia nchi zinazotuzunguka kama Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji na Congo huko dola haijashuka na sehemu iliposhuka imeshuka kwa asilimia chache sana kulinganisha na nchini. Kumbe kipi kimefanyika nchini hadi dola ishuke na shilingi ya Tanzania ipande thamani?.
Kuna sababu nyingi ila sababu kubwa ni
1. Sera za kifedha za benki kuu ya
Tanzania
2. Kupunguza uhitaji wa dola.
Kwa muda sasa benki kuu ilikataza matumizi au malipo ya dola
kwenye biashara za ndani. Hali hii imepelekea ongezeko la dola na kufanya
ishuke thamani.
3. Kuongezeka kwa upatikanaji wa dola.
Kuna njia tofauti tofauti ambazo nchi hupata dola ama fedha
za kigeni . Njia hizi ni kama kuuza bidhaa nje, utalii, mikopo na misaada.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la sekta ya utalii hali ambayo imeongeza upatikanaji
wa fedhs za kigeni na kulingana na Sera
za benki kuu watalii hawa wanatakiwa walipe malipo kwa shilingi ya Tanzania
hivyo dola zinabaki benki.Hili linaongeza upatikanaji wa dola zaidi na kuifanya
ishuke thamani.
FAIDA NA HASARA ZA KIUCHUMI ZITOKANAZO DOLA KUSHUKA THAMANI
Kushuka ama kupanda kwa dola ni kama pande mbili za sarafu kuna faida na hasara zake. Siku zote kiuchumi huwa tunafanya kitu ambacho faida ni kubwa kuliko hasara.
HASARA
Kwa nchi ambayo uchumi wake hutegemea zaidi kupeleka bidhaa
nje ( export) mfano China au Ujerumani hupendelea zaidi dola ipande thamani
zaidi,ili bidhaa zake ziwe bei chini na kuvutia wateja na wawekezaji zaidi.
Kushuka kwa dola kuta athiri biashara zote zinazopelekwa nje
ya nchi kama bidhaa za uvuvi, kilimo au madini. Kwakuwa watu hawa watapata
faida kidogo ukilinganisha na awali na bidhaa husika zitakuwa na bei kubwa
kwenye soko la dunia hivyo kuwa na ushindani mdogo. ( low compititive
advantage)
FAIDA
Waswahili wanasema kifo cha panzi furaha kwa kunguru. Kwa
zile biashara zinazoagizwa kutoka nje kama bidhaa kutoka China, magari kitoka Japan
ama mashine kitoka Ujerumani. Hawa wote
watapata faida zaidi kwakua watatumia pesa kidogo kununua mzigo ule ule .Kwa
kuwa bidhaa nyingi za uzalishaji ( capital goods) hutoka nje ya Nchi .Basi, hii
itasaidia ukuaji wa uchumi na kupunguza mfumuko wa bei , sababu ya kupungua
garama za uzalishaji ( decresse in cost push inflation.
JE DOLA ITAENDELEA KUSHUKA? AU ITAPANDA
Kwa mwenendo wa sera za Marekani . Ni mapema sana kujua kitakachotokea baada ya kuapishwa Donald Trump. Japoluwa kwa sasa hadi mwezi January kuna muenendo mkubwa wa dola kushuka thamani .
Ila kwakua Trump ni kiongozi anae amini zaidi katika kuimarisha dola na katika uwekezaji zaidi , huku akiongelea mfumuko wa bei wa Marekani kuna uwezekano mkubwa wa benki kuu ya Marekani kuongeza riba zaidi . Hili Kwa mataifa makubwa zaidi kama Chins , India ama Japani inaweza pelekea Dola kupanda kwenye nchi zao ama kidunia. Ila kwa mataifa kama ya Africa itategemea sera za nchi . Kama Sera za benki kuu zitazidi kupunguza uhitaji wa dola basi . Dola itaendelea kushuka zaidi kwa Tanzania . Ikumbukwe kwamba leo hii tunaongelea kushuka kwa dola Tanzania lakini Zambia , Msumbiji, Uganda na Congo kwao dola imepanda thamani , haijshuka. Kwa sababu ya Sera za benki kuu yao
KWA UJUMLA.
kama nchi inaagiza vitu kutoka nje zaidi ya inavyopeleka nje
ya nchi( negative balance of payments), Nchii itanufaika na kushuka thamani kwa
dola. Na kama nchi inapelekea bidhaa nje zaidi, kuliko inavyo ingiza nchini( positive balance
of payments), Nchii hii itanufaika zaidi na kupanda thamani kwa dola.
Kwa kuhitimisha kabisa. Tuzidi kutumia fursa hizi za kushuka
kwa dola kuji imarisha kwa uchumi binafsi.
Nashukuru kwa kuwa pamoja nami katika makala hii na Mungu wa Mbinguni akubariki.
Asante
sana.
Makala hii imeandaliwa na
18 Comments
Maelezo mazuri japokuwa naona vyombo vingi vinaripoti kuwa dola inazidi shuka kwenye nchi nyingi hata kwenye hizo nchi ulizotaja zinazozunguka tanzania kama sikosei.
ReplyDeleteThere are some of the contries where dollar is getting stronger and some where it's not . For example in Zambia dollar is getting stronger against Zambian Kwacha
DeleteDola Ina panda na kushuka kila siku , ungejaribu kuangalia muenendo wake kwa mwezi huu wa Desemba . Tunashukuru kwa kusoma Makala🙏🏿
DeleteNimejifunza sanaa
ReplyDeleteDid learn anything brother
DeleteAsante sana kaka
DeleteTanzania vipi
ReplyDeleteIts good
DeleteTunaendelea kujenga taifa
DeleteNi jambo jema Kama umejifunza . Kukiwa na kitu kinahitaji ufafanuzi karib sana Chief
ReplyDeleteMnakaa kimya sana agroottomans ,,Kubabake Trump kazi anayoo 😀😀😀😀😀😀😀nacheka kama mazuri
ReplyDeleteTutajitaidi tusiwe kimya hivi . Kuhusu Trump Ngoja akianza io January tuone mzee
DeleteNaruhusiwa ku copy hii makala
ReplyDeleteBila shida kabisa unaweza ku copy pia uka share na Marafiki mkuu
DeletePia Kama kuna kitu ungependa kujifunza kuhusu Uchumi, kilimo ama biashara karibu
ReplyDeleteMakala nzuri sana,, vijana ni frusa kwetu
ReplyDeleteAsante sana . Hii ni kweli ni fursa
ReplyDeleteSaafi
ReplyDelete