Wengi wanaposikia biashara ama kuwekeza . Kitu cha kwanza wanasema inahitaji mtaji kiasi gani ??? Si kweli kwamba kila biashara inahitaji mtaji kufanya. Hapa unaanza kuwaza kama utani vile . Vipi nipate pesa bila kuwekeza pesa..???kwanza fikiri hili mpaka unaona sahani la wali mezani kuna mkulima Kyela alilima huo mpunga, ila lazima kuna kampuni ya mbegu ilimuuzia huyo mkulima izo mbegu na pembejeo . Bila kusahau kampuni ya usafirishaji iliofikisha mchele uliokobolewa baada ya mfanya biashara kuongeza thamani na kuhakikisha mchele unafika sokoni kwa wakati unaohitajika na mtumiaji . Huu ni mtiririko wa matukio unao tokea kuanzia bidhaa ya kilimo inatoka shambani hadi inamfikia mtumiaji mezani yaani ( Agricultural Marketing). Humo katika mtiririko huo kuna fursa nyingi mno ambazo kazi yangu leo nikukufumbua macho na wewe uzione . Aya twende kazi mkuu
Matokeo yoyote ya biashara ni bidhaa ama huduma ( goods or services). Duniani kuna nchi ambazo uchumi wake hutegemea zaidi bidhaa( production economy) mfano Ujerumani,China,Brazili, ama Agentina . Lakini pia kuna nchi ambazo hutegemea huduma zaidi( service economy), kama Marekani, Ubelgiji ,Israeli,Uhispania na Ufaransa . Ni kweli uzalishaji wa bidhaa ( goods)yoyote unahitaji pesa ( production cost) tena katika kilimo uzalishaji wowote mkubwa unahitaji mtaji mkubwa mno. Habari njema katika hili ni kwamba uzalishaji ama utohaji wa huduma ( Agricultural services) aidha unahitaji mtaji mdogo sana wa fedha ama haiitaji mtaji kabisa . Kwenye makala iliopita tulijifunza kuwa mtaji sio lazima uwe pesa . Inaweza ikawa mawazo, ujuzi ,muda, uzoefu ama taarifa . Kama sijakuacha mpaka hapo jipigie makofi . Sema nimeshatoboa maisha . Leo tunaongelea ( Agricultural services opportunities)
A. SHAMBANI
Eneo hili ndio eneo mama ambalo uzalishaji wa aina zote hufanyika . Tukisema shambani namaanisha eneo lakufugia samaki au mifugo na eneo la kupanda mazao. Shuguli kubwa inayofanyika hapa ni uzalishaji . Jiulize tu kwa haraka ni huduma ( service) gani zinahitajika hapa ili niweze kubadilisha uhitaji huu kuwa fursa ?
1. MBEGU
Kwa Tanzania kuna makampuni makubwa ya mbegu kama SeedCo,Panar,Kibo Seed na Interchick ( viranga). Makampuni haya huzalisha na kuwauzia mbegu bora wakulima . Japo kuwa kuna nakampuni mengi ya mbegu ila kuna wakulima wengi zaidi ya nusu ambao hadi leo hawatumii mbegu za dukani sio kwa sababu hawana pesa za kununua ila ni kwakuwa hawana aidha taarifa juu ya mbegu ama walipo hapafikiki kiurahisi . Mtu anaweza sema sasa apa fursa iko wapi mzee?? Fursa hapa nikuwataftia viwanda vya mbegu wakulima ambao wapo tayari kununua mbegu zao . Kama wakulima watakuwa wengi kiasi cha kushawishi kiwanda kupeleka moja kwa moja kwa wakulima wewe utakuwa kama mtu wa mauzo na kiwanda kitauza kwa bei ya kiwandani kwa wakulima wako na wewe utauza kwa bei ya sokoni baada ya kutoa gharama za usafirishaji. Hapa atakae peleka mbegu ni kiwanda ama wasambazi wakubwa . Wewe unachohitaji kufanya ni kuongea na wakulima kuwaelimisha na kuwashawishi . Hapa mtaji wako ni taarifa sahihi, wakati sahihi na kwa mtu sahihi
B. USAFIRISHAJI
5. Moja ya njia ya kuongeza thamani katika mazao ya kilimo ni kusafirisha . Yaani kutoa sehemu ya uzalishaji mkubwa na uhitaji mdogo ( low demand and surplus unit) kupeleka sehemu yenye uhitaji mkubwa ( high demand deficit unit) . Katika nchi yetu sekta hii imekuwa na changamoto kubwa hasa kipindi cha msimu wa mavuno. Wengi huwategemea madali ili kupata magari . Watu hawa kwa muda mwingine wamekuwa wakitoza wafanya biashara pesa kubwa mno kuliko uhalisia wakati mwingine . Mfano mwezi wa sita hadi wa tisa kutoa kilo moja mfano ya mahindi Mbeya hadi Dar es salaam ni Tsh. 120 kwa kilo wakati mwezi wa kumi hadi watano ni Tsh. 80 kwa kilo . Wapo watu wengi mizigo yao mingi imepotea ama kuharibika sababu ya kukosa watu waamininifu wa usafirishaji. Nadhani mpaka hapa umeshaona fursa . Kwanza unahitaji kufahamu wamiliki ama makampuni ya usafirishaji ( apa ask Mr. Google) ukishapata hili unaweza tumia hao hao madalali kupata wateja wanaohitaji usafirishaji kisha hapo utengeneze wateja wako . Kwa kila gari utakalo mtafutia mteja unaweza kupata kati ya elfu hamsini hadi laki tatu. Mfano mzuri tuu kwa mkoa wa Sumbawanga na Songwe hiki kipindi cha mavuno kuna uhitaji wa zaidi ya malori zaidi ya 50 kwa siku moja . Huu ni mfano tuu wa mikoa hio . Vipi mikoa mingine . Embu fanya uamke usingizini . Tazama fursa hizi.
KUONGEZA THAMANI

6.KUCHAKATA NA VIFUNGASHIO VYA BIDHAA YA KILIMO
Bado wakulima ama wafabiashara wengi baada ya kuchakata mazao yao mfano baada ya kukoboa mpunga wanauza vile vile tu kwenye magunia ambayo wakati mwingine yanakuwa machafu na vifungashio duni visivyo na ubora na mvuto kwa mteja ( poor convince)Kuna watu wa hali fulani ya maisha hawawezi tumia bidhaa hizi . Fursa iliyopo hapa ni katika kufanya ufungashaji( package and branding) hapa inahitaji kumshawishi mkulima ama mfanya biashara kubadili mfumo wa kuhifadhi. Mfano unaweza mtengenezea logo ili atambulike alafu kisha unaweza mshauri kutumia mfano kwa mchele ama unga ( water proof sacs) . Sasa fursa inakuaje . Apa huitaji kujua kutengeneza logo hapana . Tafuta mtu anae jua kisha ongea nae bei alafu nenda kwa mkulima ongea nae bei . Tafuta kampuni za kuprinti magunia mkulima atakupa pesa ya kununua magunia yasio na chapa( plain) alafu wewe mpe bei ya ( branded sac) alafu msaidie kufunga mfano badala ya kushona kwa mkono ashone kwa mashine . Hapa wamashine utamlipa wewe alafu wewe utalipwa na mkulima ama mfanya biashara . Kama umenipata hapa tumezungumzia fursa zaidi ya mbili.
Ukweli ni kwamba wakulima wengi huwa wanalima mazao yao na hawajui amuuzie nani . Kama ukiweza kuwataftia wakulima wateja wa kununua mazao yao basi unaweza kujiingizia kipato kikubwa . Lakini pia kuna makampuni 90 makubwa ama wagavi yanayotafuta mazao . Ukiwataftia hawa masoko basi unauwezo mkubwa wa kujiingizia kipato kwakua wahitaji wengi wa mazao wana mitaji na wana uwezo wa kuyafata yalipo . Alafu katika hili kuna mazao zaidi ya 100 unayoweza kuyafanya kuanzia nafaka , mboga mboga, matunda ,Miche ama mifugo. Changamoto kubwa ya fursa hii ni mabadiloko ya bei. Bei za bidhaa za kilimo zinabadilika kila leo kila mara ( volatility ) sasa ili uweze kujipatia kipato kupitia fursa hii ni lazima uwe na ufatiliaji wa hali ya juu sana tena wakila wakati kuhusu hali ya masoko . Kutokana na madiliko ya mifumo ya serikali unahitaji mtaji mkubwa wa watu sahihi wenye taarifa sahihi ili kufanikisha bishara katika nyanja hii.
Katika fursa ya kuunganisha wakulima na masoko ipo fursa nyingine mipakani yani kama Namanga Arusha, Mtukura Kagera, Manyovu Kigoma ama Tarakea Kilimanjaro. Katika sehemu hizi kuna wakulima huitaji kusafirisha mizigo yao ama kutafutiwa wateja wa mazao yao . Unaweza toa huduma ya kuwasidia kwa kuwaunganisha na ma ajenti wavushaji ama wateja wanunuzi na wewe ukalipwa ( marketing fee) . Katika sehemu hizi masoko ni makubwa na mazao ni mengi mno unaoweza kuyafanyia kazi . Jaribu uwe na ufatiliaji tu , utanishukuru badae.
9. MTANDAO
Katika zama tunazoishi ( information age) kuna ukuaji mkubwa wa usaambaaji wa taarifa kwa njia ya mtandao. Kila leo watumiaji wa mtandao wanazidi kuongezeka . Mtandaoni inakuwa ni sehemu rahisi sana kupata wateja mbalimbali. Fursa hii unaweza itumia kwa kutumia kutangaza fursa zote tulizojadili hapo juu . Mtandaoni unaweza tangaza bidhaa za kilimo za watu wengine ama bidhaa zozote alafu ukaweka na bei ( marketing fee) yako ili uweze kupata faida. Hii njia skuizi wengi hutumia kwenye nguo na simu. Sasa unaweza tumia kwenye bidhaa za kilimo . Ugumu wake ni kwamba tofauti na nguo ama simu zenye bei isio badilika badilika .Bidhaa za kilimo zina badilika mara kwa mara . Hivyo unahitaji kuwa mfailiaji mkubwa mno.
Tunashukuru sana kupitia makala hii. Ubarikiwe sana .
Erick Muhini ( Agro Economist)
Wasiliana nasi kupitia:
+255744207795
BONYEZA HAPA kuwasilia nami whatsapp
ReplyForward |
7 Comments
NIMEJIFUNZA KITU KWA KWELI
ReplyDeleteThat's s great brother . Share it with friends as well
Deletewoow very fantastic ,nimeshare makala hii ubarikiwe uliyeandika
ReplyDeleteThat's great Alice . Blessings
Deletegreat tuna kitu kikubwa cha kujifunza hapa
ReplyDeleteMakala nzuri sana
ReplyDeleteSisi ni wadau wa kilimo ,Tunatamani kuunganisha mawazo pamoja ,mnapatikana wapi?
ReplyDelete