Ticker

6/recent/ticker-posts

USIPOZINGATIA HAYA HUWEZI KUIPATA MALI SHAMBANI

 

Watu wengi hudhani wakiwa na mtaji na masoko ya uhakika watafanikiwa kwenye kilimo . La hasha . Hata kama una mtaji wa kutosha na masoko ya uhakika , Usipozingatia yafuatayo kamwe huwezi fanikiwa kwemye kilimo biashara 

Tunaposema " kilimo"mara nyingi watu hulenga uzalishaji wa mazao na ufugaji wa wanyama, lakini kilimo kinahusisha pia uvuvi wa samaki pamoja na uuzaji wa bidhaa zinazotokana na shughuli hizo.

Lakini siku ya leo tunapozungumzia kilimo tunalenga/ tunamaanisha uzajishaji wa mazao. Tunaposema mafanikio kwenye kilimo wengi tunamaanisha maendeleo yatokanayo na kilimo ambayo ni pamoja na kukua kwa uchumi kwa ujumla, lakini kwa mkulima mafanikio ya kilimo kwakwe sio kupata pesa nyingi tu baada ya mavuno bali pia kuwa na furaha au faraja anapotazama shamba lake jinsi mazao yalivyonawiri vizuri, kwani ndio mwanzo wa mavuno mengi pamoja na pesa baada ya kuuza mazao hayo.

Mpenzi msomaji, naimani umewahi sikia au kusoma sehemu mbalimbali kwamba "kilimo kinaanzia sokoni", na sio shambani. Kauli hii inaukweli ndani yake, lakini unatakiwa ukumbuke kuwa hata kama una uhakika wa masoko ya mazao yako, pamoja na mtaji wa kutosha kwa ajiri ya kilimo, Kuna mambo ya msingi usipozingatia huwezi kupata mafanikio kwenye kilimo ( crop production).

1.Ardhi

2.Mbegu bora

3.Afya ya mmea

4.Muda sahihi

5.Kuhifadhi

1. Ardhi

Ardhi ni (growth media) ambayo hutumika kukuzia mmea, kwani husaidia kuupa mmea virutubisho, maji pamoja na hewa.

Kuna mambo makuu mawili ya kuzingatia kwenye swala la ardhi ya kilimo.

Kwanza ni kuchagua ardhi yenye rutuba na inayoruhusu zao husika kukua vizuri. Kwakufanya hivi itasaidia mazao yako kukua vizuri bila changamoto zozote, kwani kila zao linakua vizuri kwenye aina fulani ya ardhi kwa mfano viazi Mviringo vinastawi vizuri kwenye ardhi yenye tifutifu inayoruhusu hewa kupita, na sio kwenye udongo wa mfinyanzi kwa sababu hairuhusu kiazi kutanuka vizuri na kuwa na umbo nzuri.

Pili ni kuandaa ardhi vizuri kabla ya kupanda zao lolote, kulima ( tillage). Hii husaidia kuboresha ardhi na kutengeneza mazingira mazuri kwa ajiri ya mbegu kuota na kukua, pia kulima kunisaidiaa mzunguko mzuri wa hewa kwenye udongo, mmea unapata maji vizuri na mizizi inakuwa vizuri pia kulima kunasaidia udongo kupata joto la kutosha kwa ajiri ya ukuaji wa mmea.

2. Mbegu bora.

Baada ya kuchagua ardhi inayofaa na kulima vizuri, ni muhimu pia kufanya maamuzi sahihi unapofika muda wa kuchagua mbegu. Inashauriwa na muhimu kuchagua mbegu bora ambayo inatoa mazao mengi na inauwezo wa kuhimili ukame, magonjwa pamoja na hali mbaya ya hewa. Hii itasaidia kupunguza gharama za kutibu mmea mara kwa mara na mkulima atapata mazao mengi zaidi.

3. Afya ya mmea


Mmea wenye afya nzuri ndio wenye uwezo wa kutoa mazao mengi mwisho wa siku. Asilimia kubwa ya upotevu wa mazao unatokana na afya duni ya mmea. Tunapozungumzia afya ya mmea tunamaanisha vitu vifuatavyo.

Kwanza, mmea unapata virutubisho vyote kwa ajiri ya ukuaji wake kwa mfano NPK (Nitrogeni, phosphorus na Potassium) na madini mengine kwa mfano madini ya chuma na kadhalika. Madini haya ni muhimu sana kwa ajiri ya afya ya mmea, mara nyingi ardhi huwa na madini haya yote ( Macro and micro nutrients), lakini mda mwingine inatupasa kutumia mbolea kwa usahihi ili kuhakikisha mmea unapata virutubisho hivyo.

Pili ni Udhibiti wa unyevu, mmea hukua vizuri katika kiwango cha wastani wa unyevu. Kwahiyo ni muhimu kuhakikishaa mmea unapata unyevu wa kutosha, kwani unyevu uliozidi huathiri ukuaji wa mmea pia mmea hauwezi kukua vizuri kwenye ukame uliopitiliza, kwahiyo ni muhimu kutumia njia mbalimbali kuhakikisha mmea unapata unyevu wa kutosha njia hizo ni pamoja na kilimo cha umwagiliaji, kuweka matandazo na kupanda miti ya kivuri kuzuia ukame.

Tatu, ni kudhibiti magonjwa, wadudu na magugu, kama mmea hautasumbuliwa na hivi vitu basi mmea utatumia chakula chake kwa ajiri ya kukua na kuzalisha mazao mengi, lakini mmea ukishambuliwa na magonjwa na wadudu unashindwa kukua vizuri, pia magugu kudhorotesha afya ya mmea kwa kutumia chakula cha mmea mwisho wa siku mavuno kupungua pia shamba kukosa muonekano mzuri.

4. Muda au wakati sahihi


Hapa tunamaanisha muda wa kupanda pamoja na mavuno. Muda wa kupanda una mchango mkubwa katika ukuaji wa mmea na mavuno pia, kupanda kwa wakati sahihi kuna saidia mmea kukua vizuri bila ya mashambulizi ya wadudu waharibifu tukiangalia kwenye viazi mviringo ukipanda mapema kabla ya mda wake viazi hushambuliwa na wadudu kama vile funza na kupunguza mazao.

Pia watu wengi hupuuza linapokuja swala la mavuno, lakini ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mazao mavuno kupungua na huaribika kadri yanavyobaki shambani. Hivyo ni muhimu kufanya mavuno mara tu mazao yanapokomaa kwa mfano ufuta, katanga, mpunga, matunda nakadhalika.

5. Kuhifadhi

Wakulima wengi sana wanaweza kuhakikisha mambo yote yaliyotajwa hapo juu yako sawa lakini baada ya mavuno changamoto inatokea kwenye namna ya kuhifadhi mazao. Wengi wao baada ya mavuno hawajali tena kuhusu njia bora za kuhifadhi mazao mwisho wasiku wanaishia kupata hasara kutokana na kuharibiwa kwa mazao na wadudu, kuharibika na kupoteza ubora. Hii husababisha hasara kubwa kwa wakulima.

Ukizingatia haya mambo utafanikiwa kuipata mali shambani. Bila shaka utakuwa umejifunza kitu.

Nashukuru kwa kufuatilia makala hii. Kama una swali au maoni karibu sana.

Ubarikiwe

Wasiliana nasi kupitia

info@agroottomans.com

+255 744 207 795

Husna Issa ( Agro Economist)

Post a Comment

9 Comments

  1. Umenena vyema huku kwetu watu wanapata hasara sana ya uhifadhi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana kwa kufatilia makala zetu endelea Kushare na wengine

      Delete
  2. Asante sana kwa elimu nzuri

    ReplyDelete
  3. Kichwa chenye maarifa mbarikiwe sana agroottomans team

    ReplyDelete
  4. makala nzuri nimesoma mara mbilimbili mwenye masikio na mwenye macho asome

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete