Ticker

6/recent/ticker-posts

HEAT STRESS(Shinikizo la joto ) LINAVYOWEZA KUATHIRI UZALISHAJI WA MAZIWA KWA NGOMBE NA NJIA ZA KUZUIA ATHARI HIZO

 

HEAT STRESS IN A DAIRY COWS (Shinikizo la joto)

Hili ni moja ya tatizo kubwa ambalo hutokea kwa ngombe wengi, hasa wakati wa kipindi cha joto. Tatizo hili mara nyingi huwa linamfanya ngombe kuwa na joto kubwa la mwili ukilinganisha na joto lake la kawaida. Tatizo hili hupelekea ngombe kupunguza uzalishaji wake kwa mfano ngombe atapunguza kiasi cha maziwa ambacho anatakiwa kutoa kila siku, pia inapunguza uwezo wake wa kuzaa (fertility) kwa ngombe husika.

 

Leo tutaangalia na kuongelea upande wa kuzalisha maziwa

 

Hapa nisikilize kwa makini nataka kukuambia kwanini ngombe atapunguza uzalishaji wa maziwa akipata na heat stress…..

 

Ni kitu kidogo tu na cha kawaida sana. Pale ambapo tu joto linaongezeka ndipo hapo hapo ngombe anapunguza ulaji wa chakula na anapopunguza ulaji wa chakula ndipo tunapata kitu kinaitwa low forage intake, yaan lishe duni kwa ngombe ambapo hii itapelekea kwenye rumeni ya ngombe kuwa na hali ya acid nyingi na kupunguza fat contents of milk  ambapo moja kwa moja itapelekea kupunguza uzalishaji wa maziwa. Kwa sababu, hizo fat content of milk ndo zinazohusika moja kwa moja kwenye uzalishaji maziwa ya ngombe

 

Sasa twende pamoja tuone nini kinatakiwa kifanyike ili kuweza kuwaondoa ngombe na hili hali ya heat stress………

 

Vitu unavyotakiwa kuvifanya ili usiingie kwenye athari la ongezeko la joto ni kama ifuatavyo

·        Kuwaongezea kiwango cha maji wanayokunywa kila siku. Hii ni muhimu sana kwa sababu maji yatapooza joto la mwili kwa haraka sana hivyo ni muhimu sana kuwaongezea kiwango cha maji wanayokunywa. Hii hufanyika vipi sasa? Waongeze vifaa vya kuwekea maji ya kunywa kwenye zizi lao, kama wnaafuata maji ya kunywa umbali mrefu basi wapunguzie huo umbali maji yawe karibu yao Zaidi.

 

·        Kuwe na tabia ya kuwanyunyuzia maji ngombe wako kwenye miili hasaa wakati wa jua linapowaka hii itawasaidia ngombe kupooza miili yao na kubaki na joto lao lile la kawaida. Hapa kuna vifaa maalum ambavyo vinatumika kwa ajili ya kuwanyunyuzia maji.

 

 

·        Ujitahidi banda lako liwe na muingiliano mkubwa wa hewa kwa sababu kama muingiliano utakuwa mdogo hii itapelekea hewa iliopo ndani kuwa ya moto hivyo kufanya banda zima kuwa na joto na hivyo ngombe watapandisha joto lao la mwili

 

·        Pia unashauriwa kuweka feni ndani ya zizi lako kama mifugo yako haitoki nje kwa siku nzima. Feni hizi zinatakiwa kuwashwa pale tu ambapo unaona joto limekuwa kali ndani ya zizi na hii hutokea mara nyingi wakati wa mchana ambapo jua linawaka.

 

·        Epuka kuwafanyia chanjo za mara kwa mara kipindi cha joto. Hii inamaanisha unatakiwa kuwa makini sana kipindi cha joto ili kuwaepusha ngombe wako na magonjwa na kuwaepusha kwenye swala la kuwapa chanjo za mara kwa mara. Kwa sababu chanjo zinapelekea joto la mwili kupanda.

 

·         Kitu kingine ni kuwa na mazoea ya kuwapima joto la mwili mara moja kwa wiki ili kuona hali ya joto ya miili yao inavyoenda na kujua kama njia ambazo unazitumia kushusha joto la mwili kama zinafanya kazi.

 

·        Mwisho kabisa na ndicho cha umuhimu sana kwa ajili ya kuzalisha maziwa ni swala la kubalance vyakula katika kipindi hiki cha joto. Mwanzo kabisa tuliona kwamba mifugo itapunguza kula chakula wakati wa kipindi hiki cha joto na kupelekea kupunguza uzalishaji wa maziwa ,hivyo basi tukiweza kubalance vyakula kwenye kipindi hiki cha joto basi tutaepuka athari ya kupungua kwa maziwa kwenye kipindi hiki cha joto. UNAWEZA KUJIULIZA SASA HAPA TUNAFANYAJE…….Sikia ipo hivi kuna vitu vitatu hapa vya umuhimu ambavyo tunaweza kufanya kwenye swala la chakula.

                         Kwanza kabisa ujitahidi kwa wakati wa joto kuwapa mifugo chakula chenye quality ya juu kabisa ile quality ya kwanza kabisa kama ni majani mabichi basi ujitahidi uwape yale mazuri kabisa kwa sababu anakuwa amepunguza hamu ya kula kwa hiyo lazima tumpe chakula kizuri sana ili aweze kula Sanaa. Na hapaa tutakuwa tumeipunguza ile hali kuwa mifugo kuwa wanapata LOW FORAGE INTAKE ambayo tuliona mwanza kabisa wa Makala hii. Hapa tunasema mifugo wanatakiwa kupata HIGH QUALITY FORAGE

                        Wapewe chakula cha jamii ya nafaka, hii ni muhimu kwa sababu aina hii ya vyakula huwa na kazi ya kuzalisha nguvu(ENERGY) mwilini, nguvu hiyo itatumika kwenye uzalishaji wa maziwa kwa ngombe.

                       Mwisho ni inabidi kufanya nyongeza ya fats content kwenye lishe yao ya kila siku. Kama tulivyoona kwenye kipindi hiki cha joto kutakuwa na upungufu wa fats contents ambazo zinahusika moja kwa moja kwenye uzalishaji wa maziwa. Kwahiyo ni muhimu sana kufanya nyongeza ya fats kwenye lishe yao ya kila siku ili kufidia ule upungufu ambao unatokea.

 

Kwakufanya hayo yote lazima utaona matokeo kwenye mifugo yako hasa kwa wakati huo wa joto.

 

ASANTENI NA KARIBUNI KUENDELEA KUFUATILIA UKARASA WETU NI MATUMAINI YETU MNAJIFUNZA MENGI KUPITIA UKURASA HUU. KAMA UNATAKA KUJUA ZAIDI AU KUELEWA ZAIDI TUPIGIE SIMU AU KUTUMA UJUMBE KWENYE MITANDAO YETU YA KIJAMII.

PIA TUNAKARIBISHA MAONI NA MAPENDEKEZO MNATAKA TUONGELEE KITU GANI KWENYE MAKALA ZIJAZO ILI MUENDELEE KUJIFUNZA ZAIDI.

Post a Comment

0 Comments