Hakuna kitu kizuri kama kula chakula ulicholima mwenyewe ,Siku hizi kumekuwa na changamoto kubwa hususani kwenye matunzo na makuzi ya mboga mboga na matunda ,watu wengi wamekuwa wakizikuza kwa kutumia madawa makali pamoja na kemikali ili kuleta matokeo ya haraka ,jambo ambalo limeleta madhara kwenye afya za watu wengi
Je umekuwa ukisumbuka unatamani kulima? ila changamoto ya eneo imekuwa ikikusumbua sana na kukukatisha tamaa ya kuanzisha bustani ya mbogamboga na matunda
Leo nipo hapa kukuondoa hofu kuwa kilimo kinawezekana ukiwa sehemu yoyote labda usiamue tu
Tumia mifuko iliyojazwa udongo na mbolea kulima,pia waweza tumia makopo au ndoo zilizotobolewa kuoteshea mboga mboga na matunda
Endelea kufuatilia Tovuti yetu ,makala ijayo Tumekuandalia somo zuri ,jinsi ya kuandaa bustani kwa kutumia mifuko, endelea kufuatilia tovuti hii usipitwe na mambo mazuri
1 Comments
Tunasubiri makala kwa hamu
ReplyDelete