Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUANDAA BUSTANI YA MBOGA MBOGA MBOGA KWENYE MIFUKO

Mfuatiliaji wa Agrootomans ,Tunayofuraha kuwa nawe siku ya leo tena 

Kama tulivyokuahidi katika makala iliyopita makala iliyokuwa inasema 

UFINYU WA ENEO USIKUFANYE USHINDWE KUFANYA KILIMO

Leo tumekuletea makala nzuri kabisa itakayokuwezesha kufanya kilimo kwenye ufinyu wa eneo au sehemu isiyo na nafasi ya kutosha

JINSI YA KUPANDA MBOGAMBOGA KWENYE MFUKO

Andaa mashimo ya mstatiri pembezoni mwa mfuko. Kwa kukata pande tatu za mstatiri na kuacha sehemu ya juu, unaweza kufunua na kufunika shimo na hivyo unaweza kupanda mbegu au mche chini ya mfuniko huo wa shimo. Mfuniko huo katika shimo hufanya mche kukua kuelea pembeni na sio juu

Mboga kama nyanya, spinachi, kabichi, swiss chard, pilipili, hoho bamia , matango beetroot n.k zinaweza kulimwa katika kilimo hiki . Mboga zenye mizizi mirefu kama matango zinaweza kulimwa katika sehemu ya juu pekee. Mboga zenye mizizi mifupi na inayokuwa wima bila kuhitaji msaada kusimama inaweza kulimwa kwenye shemu za pembezoni mwa mfuko . Mboga hizi ni kama pilipili, Spinachi, beetroot, kabichi ya kichina na viazi vitamu


Kuandaa mashimo


Kwa mimea yenye mizizi mirefu kama matango, shimo linapaswa kuandaliwa juu ya mifuko na mbolea inapaswa kuongezwa. Panda mbegu moja au mbili au mche mmoja au miwili. Baada ya siku chache, ondoa magugu na mimea dhaifu ili kuongeza nafasi na uzalishaji

 Kupanda miche



Miche inapokuwa na umri wa mwezi mmoja hivi, inafaa kupandiza katika mashimo ya mstatiri pembezoni mwa mifuko. Nafasi za miche hutegemea aina ya mimea, ingawa nafasi ya sm 20-25 mstari hadi mstari na sm 20-25 mmea hadi mmea inaweza kutumika. Kama mimea imepandwa kwa nafasi finyu mazao hupungua

Kuweka mbolea



Pamoja na mbolea ya mboji na samadi, unaweza kuweka mbolea za viwandani kama UREA na booster. Kiwango kinategemea aina mboga na mahitaji lakini kiwango cha kawaida ni UREA gramu 15 na zile za booster soma maelekezo kutoka kwenye mbolea yenyewe

Umwagiliaji



Ili kuhakikisha mimea inakuwa na afya, mwagilia lita 1-2 za maji juu ya mfuko kila siku jioni. Kuweka mtandazo ya majani makavu juu ya mfuko hupunguza upotevu wa maji na huhifadhi unyevunyevu kwa muda mrefu. Hii ina maanisha kiasi kidogo tu maji kitahitajika kwa mimea yako

N:B Mbinu hii inafaa pia kutumika kupanda mbogamboga katika makopo ndoo na madumu


Asante kwa kufuatilia makala hii usiache kutoa maoni yako hapa chini



Post a Comment

2 Comments