Ticker

6/recent/ticker-posts

ATHARI ZA MIGOGORO ILIYOPO KIDUNIA KWENYE UCHUMI WA DUNIA NA KILIMO BIASHARA ( EFFECT OF CURRENT WORLD CONFLICTS TO THE WORLD ECONOMY AND WORLD  AGRIBUSINESS SYTEMS)

                                    
Bila shaka ukifungua televisheni yako kwa sasa mambo mengi utayosikia ni vita ya Israeli na Hamas , Vita ya Ukraini na Urusi , Mapinduzi ya Africa Magharibi , Vitisho kati ya China na kisiwa cha Taiwani, Korea kaskazini kujaribu makombora ya masafa marefu ( inter continental ballistic missiles), Vita ya Kibiashara kati ya China na Marekani ama vita ndani ya nchi ya Sudani. Haya yote pamoja na mengine mangi yanatokea ulimwenguni kote .

Vita ya aina yoyote inahitaji fedha kubwa kwa mfano mdogo tu nchi ya Israeli inatumia zaidi ya dola za kimarekani 50,000 ( zaidi ya 110,000,000 ya kitanzania) kutegua kombora kwa mfumo wake wa ( Iron dome sytem) ama kombora  moja la kawaida tu linagharimu zaidi ya dola za marekani 3500 ( zaidi ya 8,000,000 ya kitanzania ).

Huu ni mfano mdogo tu .

Kwa takwimu za sasa zaidi ya asilimia 2 (more than 2% of world GDP) za pato la dunia zinatumika katika ulinzi na takwimu zinazidi kuongezeka  tangu vita ya Urusi na Ukraini ianze .



Ikumbukwe kwamba japo kuwa machafuko mengi husababisha hasara kwa serikali nyingi ila kuna serikali nyingi zinanufaika na machafuko hayo kwa kuuza silaha za kivita. Mfano mdogo tu ni Irani  imeongeza mauzo ya ( drone) kwa Urusi tangu vita ya Ukraini ianze. Ama marekani iliongeza uuzaji wa silaha Saudi Arabia kipindi cha uhasama kati ya Iraq ( suni) na  Saudi Arabia ( Shiha).

Katika historia  baada ya vita ya kwanza ya dunia ya mwaka 1914 kilichofata miaka 15 baadae ilikuwa ni anguko kubwa la kiuchumi wa dunia  ( Great Economic depression).

Hapa turudi darasa la uchumi kidogo .

Moja ya sheria kubwa inayo ongoza uchumi wote ni sheria ya uhitaji na ugavi ( demand and supply law).

Kila kimoja kinamtegemea mwenzake yani,

Ugavi (Supply) inategemea uhitaji uliopo ama demand kwa lugha nyingine . Uhitaji wote kwa ujumla unaitwa '' public spending " na kinachochochea uhitaji huo ni " government spending " ama matumizi ya serikali. Kama matumizi ya serikali yatakwenda kwenye vitu ambavyo havipeleki pesa mikoni mwa watu tutapata " supply and demand mismatch" yaani bidhaa zitakua nyingi na pesa chache. Hii itapelekea kuwa na "deflation " kiuchumi hii ina athari zake. Hali kama hii imetokea China. Jambo kama hili lita athiri ile nchi iliyotumia pesa nyingi kuagiza bidhaa nje ya nchi, mfano silaha ( one of government spending).

Kwa ile nchi iliyouza silaha itakuwa ni stori nyingine kabisa ongezeko la pesa nyingi kuliko uhitaji. Ongezeko hilo la pesa linaweza kusababisha ( demand and supply mismatch) ambayo ni "inflation "  ambayo ni kinyume na hii ya kwanza, hii inakuwa ni fedha nyingi bidhaa kidogo. Hali kama hii imeikuta nchi kama Marekani hivi karibuni.

Kama tumeelewa kidogo mpaka apo tutoke sasa kwenye darasa la uchumi tuje kwenye mada kuu.

Bila shaka haujabaki Chalinze sote tumefika Mbezi. Usichoke twende pamoja mkuu.

JE, KUNA ATHARI GANI KWENYE UCHUMI WA DUNIA ZINAZOWEZA KUSABABISHWA NA MIGOGORO AMA VITA ZINAZOENDELEA SASAIVI BAINA YA NCHI NA NCHI ????

Uchumi wa dunia unaendeshwa na biashara zinazotokea baina ya nchi na nchi kadri ya uzalishaji na uhitaji wa nchi  husika.

Uzalishaji ukiwa mkubwa kuliko uhitaji bidhaa husika zitashuka thamani na pesa za nchi inayozalisha ( exporting country)  zitapungua uwezo wa kununua ( decrese in purchasing power) wakati pesa za nchi inayonunua ( importing country) itaongezeka uwezo wa kununua ( increase in purchasing power) sikuwa na lengo la kukumbusha International trade lakini huu ndio uhalisia.



Apa vita zinazoendelea zina athiri vipi uchumi?

Tuchukulie mfano mdogo tuu.  Siku ya Jana (21.10.2023) Raisi wa  Marekani J. Biden aliomba apatiwe dola za kimarekani billioni 100 kwa jili ya kusaidia Ukraini na Israeli. Hizi pesa zina athari ipi kwa uchumi wa dunia??. Pesa hizi kama zinatumika katika vita zinakwenda kuongeza mzunguko wa pesa kwenye uchumi wa dunia kwa kupitia sekta ya ( industrial millitary complex) kama tulivyona kama ni lazima uhitaji ndio uongoze uzalishaji , pesa hii inapowekwa katika mzunguko ina sabisha ongezeko la mfumuko wa bei ki dunia ( increase in world inflation) pengine unaweza sema ni kwanini?? Sababu ni ile ile ambayo ni " pesa nyingi kuliko bidhaa" ( a lot of money few goods) na hali hii imetokea kipindi cha Uviko- 19 serikali ya Marekani ilivyozalisha ( print) pesa kufufua uchumi uliozorota (economic stimulus) .

Ikumbukwe kwamba bado uchumi wa dunia ulikuwa katika hali ya kujikwamua kutoka uzorotaji uliosabishwa na Uviiko-19.

Lakini hiyo ni moja tu ya athari mfano vita ya kibiashara ya China na Marekani inayosabishwa kutokana na kuongezeana kodi bila msingi, kunapelekea athari kubwa kiuchumi. Mfano kodi inaongeza gharama za uzalishaji ( incresed in production cost) hii inatengeneza " cost push inflation.  Na kwakua hawa ni wazalishaji wakubwa kidunia uchumi wote wa dunia unazorota kwa sababu za kisiasa ambazo hazikuwa na ulazima kiuchumi.

Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa " induced demand" huu ni uhitaji ambao unasabishwa na kitu fulani ila kimsingi haukuwepo. Mfano  ukihisi  bei ya unga itapanda kesho utahakikisha unanunua ata unga wa miezi mitatu . Sasa hili swala ni kubwa sana  hasa kwenye vita.  Changamoto la hili linaweza kuongeza ama kupunguza uhitaji wa bidhaa fulani hasa wakati wa vita. Ni kama vile barakoa zilivyopanda bei kipindi cha Uviko-19.  Kwa kifupi vita inasabisha" world  trade distortions.". Ambayo hii inaweza sababisha anguko la uchumi wa dunia.

Lengo langu si kukuchosha mada hii ni pana kidogo nadhani kabla hujaanza kusinzia ngoja tuhamie kwenye kilimo biashara kidogo kisha nikuache upumzike.

 

HIVI KILIMO BIASHARA KINAWEZA KU ATHIRIKA VIPI KUTOKANA NA VITA PAMOJA NA MIGOGORO ILIYOPO HIVI KARIBUNI.??

Moja ya athari kubwa inayoweza kusababishwa na vitakwenye kilimo biashara ni kuharibika kwa mfumo wa uhitaji na ugavi unaopelekea anguko kubwa la bei. Mfano mdogo tu ni  baada ya Urusi kujitoa katika ( Red Sea grain Deal ) miezi miwili iliyopita nchi ya Ukraini ilitaka kuuza ngano yake katika nchi za Ulaya kitu kilichopeleka kuwaweka wakulima wa bara  la Ulaya  katika hatihati ya kupata hasara kwa sababu mzigo mwingi wa bei ndogo kutoka Ukraini ulipoingia sokoni.

Kwa nchi kama Sudani ambayo huzalisha zao la ufuta kwa wingi vita imepelekea bidhaa hii isifike sokoni hii linapelekea ( supply shock) ambapo kwa muda mrefu ( long run)  imesabisha ongezeko la bei ya zao la ufuta katika soko la dunia.

Kwa nchi za Africa ya Magharibi ( Ecowas) ambazo huzalisha mazao kama Cocoa ama mafuta ya mawese.  Migogoro ya kiuchumi inapelelekea uharibifu wa mfumo wa uzalishaji na uchakataji , jambo ambalo litapelekea ( shortage in supply at constant demand) ongezeko la bei ya bidhaa hizi katika soko la dunia . Na hata itakapoisha hiyo migogoro wanunuzi wengi itawachukua muda kuamini kuzalisha bidhaa hizo katika maeneo yao .

Lakini kwakua kilimo biashara kinategemea sekta nyingine kama sekta ya nishati hasa katika uzalishaji na uchakataji . Migogoro mingi ama vita zinapelekea ongezeko la bei ya nishati kama mafuta ( petrollium product). Hili imetokea takribani miezi miwili iliopita kipindi nchi zinazozalisha mafuta yaani (OPEC+) kupunguza uzalishaji kwa makusudi ili kuongeza bei ya mafuta ama G7 kuzuia ununuzi wa mafuta ya Urusi( induced supply shock). Haya yote yanao geza gharama za uzalishaji wa bidhaa za kilimo na hii inapelekea ( cost push food inflation). Hali hii inafanya maisha ya watu yazidi kuwa magumu na pesa kupungua uwezo wake wa kununua sababu ya mfumuko wa bei za vyakula ( Increase in food inflation). Jambo kama hili linaweza kupelekea hadi kuzorota kwa afya sababu ya mlo duni na kuongezeka kwa hali ya umasikini ya kidunia.

Lakini wataalamu wa mambo wanasema kila tatizo ni fursa.

KAMA KIJANA MTANZANIA UNAWEZA KUTUMIA HAYA KAMA FURSA  ????

kama tulivyojadili huko juu. Kwa nchi kama Tanzania tunaweza tumia kama fursa . Mfano katika kuongeza uzalishaji kwa mazao yalio ongezeka uhitaji, hii inawezekana kutokana na eneo tulilopo ki jeografia , amani tulionayo , ardhi kubwa inayo weza tumika kuzalisha na hali ya hewa nzuri.

Uzalishaji wa mazao yanayoweza kupanda bei ni kama michikichi  ,ufuta, cocoa na mimea jamii za mikunde. Kunaweza kutupa nafasi nzuri na faida kubwa kwa kufidia ( decreased in supply) ama kupungua kwa uzalishaji hasa kwenye sehemu zenye migogoro.

                                     


Tunashukuru sana kwa kupitia makala hii.

Mungu wa Mbinguni Akubariki sana . 🙏🏿🙏🏿🙏🏿

 

Na Muandishi wako Erick Muhini ( Agro Economist)

 

Wasiliana nasi kupitia :

+255744207795

Info@agroottomans.com

Post a Comment

6 Comments

  1. Kutoka ikungi Singida nawapata sana Ottomans ,toka nifuatilie blog yenu nimeongeza kitu,huku kwetu Singida tumeiona fursa kwenye ufuta ,tuna lima kama vichaa

    ReplyDelete
  2. Hii makala imeenda shule asante mwandishi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shukrani kaka endelea kufuatilia makala zetu 🙏🙏

      Delete
  3. Congratulations are in order, very educative

    ReplyDelete