Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIFAHAMU CHANGAMOTO UNAZOWEZA KUKUTANA NAZO NA NAMNA YA KUZITATUA UTAKAPO AMUA FANYA KILIMO BIASHARA KIMATAIFA.

Kilimo ni biashara kubwa ambayo huyaingizia mataifa mengi pesa za kigeni . Sekta hii hutoa ajira kwa vijana wengi katika hasa mataifa yanayo endelea kiuchumi. Biashara ya kilimo huusisha sekta nyingine tofauti tofauti kama uchukuzi, sekta za fedha, sayansi na teknolojia. Kuna fursa kubwa katika kufanya biashara kimataifa hasa katika mataifa yenye uzalishaji mdogo wa mazao husika. Katika kufanya kilimo biashara  kimataifa kuna changamoto mbali mbali ambazo mtu anaweza  kukutana nazo. Changamoto hizi ni kama zifuatazo.

1. Gharama  za Ubadilishaji wa fedha ( exchange rate)

Mara nyingi  unapotoa bidhaa yako kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine hasa za kilimo kuna aina mbili unaweza ukauza bidhaa hii. Kwanza unaweza kutumia pesa ya nchi husika ama ukatumia pesa ya kimataifa ambayo kwa sasa inatumika zaidi dolla ya marekani , Yuro ya ulaya, Yeni ya Japani na Yuani ya China. Ambapo kwa sasa inatumika zaidi dolla ya marekani .Ama unaweza tumia pesa ya nchi husika yani ( bilateral currency exchange)
a)Pesa ya kimataifa ( dolla)
Mpaka kuandikwa kwa makala hii dolla ya marekani ndio pesa inayotumika zaidi katika biashara za kimataifa . Hili swala hufanya thamani  ya dolla kupanda na kushuka kadiri ya uhitaji . Unaweza peleka mazao yako mathalani Ulaya pindi mzigo upo njiani bei ya dolla katika soko la dunia ikashuka hii inaweza kukupelekea kupata hasara.
Kipi kifanyike ili kukusaidia katika hili ??
Kabla hujapanga kufanya biashara kimataifa hakikisha umefanya utafiti yakinifu kujua mwenendo wa dolla katika soko la dunia. Kisha lazima ujiwekee kiasi ambacho hata kama dolla itashuka bado hautapata hasara yani kitaalamu ( sensitivity margin). Hivyo kama  hujaamua fanya haya . Tafuta mchumi kilimo wa kukusaidia ama kukushauri.

b) Fedha za nchi husika ( bilateral currency trade)

Aina hii ya biashara haikupendelewa sana kutumika kabla ila sasa inakuja kwa kasi . Hii inahusisha kubadili fedha moja kwa moja bila kuhusisha dolla. Tumeona sasa nchi kama Urusi na China , Urusi na India ama China na Brazili wakifanya aina hii ya biashara. Changamoto kubwa ya kilimo biashara katika mfumo huu ni pale ambao nchi moja inakuwa na fedha ambayo haina uthamani halisi ( over or under valued currency) Kitaalamu huwa tuna tumia njia inayoitwa ( big mac index ) kutambua hili .Mfano ulio dhahiri utaupata kama utatoa bidhaa yako ya kilimo toka Tanzania kwenda Burundi.  Thamani inayosemwa kibenki ni tofauti kabisa na uhalisia uliopo sokoni .
Pia pesa kati ya nchi na nchi hutegemea uhusiano wa kiuchumi na  kibiashara kati ya nchi hizi . Hili hufanya pesa katika nchi husika kupanda na kushuka kwa haraka ( volatility) hali hii inaweza kukupa hasara kubwa hasa pale utakapo peleka zao lako alafu kipindi unauza ,thamani ya pesa husika ikashuka. Mfano mzuri ni kwamba umetoa mchele Kyela Mbeya ukapeleka Lusaka Zambia ,muda upo Zambia unauza bei ya kwacha inashuka ,kulinganishwa na shilingi ya Tanzania hili linaweza pinguza faida ama  kukupa hasara kabisa.
Hakikisha kabla ya kuamua kufanya biashara toka taifa moja kwenda lingine umejiridhisha kuwa mkato wa pesa husika( exchange rate) hauta kuathiri hata  kama yatatokea mabadiliko ya haraka.

2. Mabadiliko ya kisera.

Kila nchi huwa na utaratibu wake wa kuingiza ama kutoa bidhaa ndani na nje ya nchi husika. Kwa kuwa bidhaa za kilimo huusisha moja kwa moja maisha ya watu serikali nyingi huziangalia ili kuzuia mfumuko wa bei , hili huwa na mkazo mkubwa kwa mazao mama ya chakula yaani ( political crops) . Mfano Tanzania mazao kama mahindi,maharage na mpunga huangaliwa kwa jicho la tatu.
Katika kufanya biashara katika nchi tofauti kuna wakati sera za nchi kuhusu kuingiza ama kutoa mazao hubadilika ghafla . Kwa mfano uliotokea hivi karibuni nchi ya Zambia kukataza mahindi yake kutoka nje ya nchi kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani na kuzuia mfumuko wa bei wa zao hilo ili kuleta usalama wa chakula ( internal food security) . Hili litamuathiri mfanya biashara wa kigeni ambae muda huo ana mzigo tayari ambao amenunua na anatakiwa akaauuze katika soko husika.
Mabadiliko mengine ya kisera yanayoweza  kumuathiri mfanya biashara wa kimataifa wa mazao ni kuongezeka kwa kodi ( tax addition) na vikwazo ( tarrif barrier). Hili tulilishuhudia mwaka jana kati ya Tanzania na Kenya katika bidhaa ya mahindi. Ama Urusi katika nafaka zake . Hii pia imeonekana katika baadhi ya bidhaa za Afrika zinazoenda Ulaya kwa habari ya mambo kama ( carbon foot print)
Hakikisha pindi hujaamua kufanya biashara katika zao fulani umefanya utafiti yakinifu ( due diligence ) kuhusu sera za kilimo za nchi husika.


3. Uhusiano wa kimataifa.

Ili nchi mbili ziweze kufanya biashara lazima ziwe na mahusiano mazuri . Kwa  mfano  .Tanzania inafanya biashara na India  sababu ya uhusiano uliopo katika  nchi hizi. Pindi uhusiano unapo badilika uhusiano unaondoka wa kibiashara . Chukulia mfano kama biashara kati ya Korea kaskazini na Korea kusini na biashara baina yao. Ama biashara kati ya Russia na Ukraine kabla  na kipindi hiki. Kwa mfanya biashara wa kilimo unaweza pata hasara pindi uhusiano kati ya nchi hizi mbili unabadilika. Hakikisha  unapotaka kupeleka bidhaa yako ya kilimo kuna usalama wa wewe kufanya biashara

4. Ubora wa bidhaa ( commodity standard )

Kila bidhaa ya kilimo inayotumika ina ubora tofauti tofauti. Hili swala ni changamoto kubwa kwa kuwa ubora wa Tanzania si sawa na ubora wa kenya mathalani . Kwa mfano Mchele unaoitwa gredi no.1 Burundi ni aina ya mpunga ambayo ni ndefu . Hata kama radha si nzuri wao watauita no.1 , kwa upande wa uganda  wanaposema huu mchele ni no. 1 wanamaanisha hauja katika katika .hata uwe punje fupi ama punje ndefu wao watauita no. 1. Kwa upande wa kenya mchele no . 1 hata kama umevunjika ila una radha watauita no.1 . Hili ni tofauti kwa Tanzania mchele ili uitwe no. 1 lazima uwe haujakatika , mrefu ama mfupi na uwe na radha .
Huu ni mfano mdogo tuu wa mchele. Unaweza amua kupeleka nyanya Afrika  kusini sababu umesikia zina lipa. Ukapeleka nyanya ndefu kumbe wao wanatumia za duara. Hii itakufanya aidha usiuze ama uuze kwa  bei ndogo kitu ambacho kitakupa hasara. Kabla hujaamua kupeleka bidhaa yako ya kilimo hakikisha unaelewa ubora unao hitajika katika soko la nchi husika ili kuepuka hasara unazoweza kupata .



5) Utapeli ( Fraud)
Utafiti kuhusu masoko ( market research) ndio kitu kikuu cha kwanza katika biashara ya kilimo ama biashara nyingine yoyote . Kwa ulimwengu tulionao sasa( information age )mara nyingi mtandaoni ndio sehemu ya kwanza kupata taarifa za awali . Huku utakutana na watu mbalimbali ambao kimsingi haufahamu undani wao. Hawa wanaweza kukushawishi ukapelekea bidhaa katika nchi fulani na matokeo yake ukapata hasara kubwa . Ili uweze kuepuka ama kupunguza kutapeliwa unapofanya biashara za kimataifa hakikisha  umefanya mambo yafuatayo .

a) hakikisha unatumia watu ama makampuni ya masoko yanayo tambulika kisheria . Kabla ya kufanya biashara na kampuni husika hakikisha umepata  taarifa ubalozini ama " chamber  of commerce " kuhusu uhalali wa kampuni unayotaka kufanya nayo kazi kama utafanya na kampuni

b) Tumia mikataba ya kisheria kila unapo toa ama kupokea pesa ama kupata kazi ya ugavi ( supply order )

C) Epuka kupeleka mzigo nje ya nchi kwenye kampuni fulani bila kupewa mkataba wa kisheria unaosimamiwa na taasisi  ya fedha ( letter of credit)

d) Epuka kufanya biashara zisizo pitia benki (cash  payment system)

e) Usiamini kiurahisi watu na uwe muangalifu  sana katika kufanya bishara katika nchi ya kigeni hasa Kwa kuepuka sehemu na watu hatarishi.

f) Jitahidi kupunguza matumizi ya madalali na hata kama unamtumia hakikisha wewe unafahamika kama mwenye mzigo

6) Usafirishaji ( Transportation)

Biashara yoyote ina sehemu kuu tatu yani uzalishaji , usafirishaji na sokoni. Usafirishaji ndio kiini cha kuunganisha uzalishaji na masoko. Bidhaa za kilimo za nafaka hazina changamoto kubwa kwenye usafirishaji kama bidhaa za kuharibika ( fresh products). Bidhaa za kilimo ambazo ni za kuharibika  huwa zinasafirishwa aidha kwa ndege ama kwa makontena yenye friji ili kuepuka kupoteza ubora . Changamoto kubwa iliopo kwenye usafirishaji ni kama ifuatavyo.

a) kwa wanaotumia usafirishaji wa magari ,gari inaweza kuharibika na mzigo ukakawia ,ama kuna wengine wamepoteza mizigo yao  baada ya madereva  kutoroka na magari .Ama gari lina haribu ubora wa mzgo . Mfano unapakia  mchele alaf gari lina tulubai linalovuja mzigo unafika umeharibika. Kujikinga na na hili jaribu kufanya kazi na makampuni ya usafirishaji yanayoeleweka na hata kama gari katafuta dalali hakikisha unamawiliano ya moja kwa moja na mmiliki wa gari ama kampuni na ufanye nao makubaliamo ya ubora na usalama wa mzigo.

b) Usafiri wa ndege huwa unakuwa na gharama kubwa . Mfano kilo moja ya parachichi inaweza gharimu(  usd 1.5- 3) kwa ndege kwenda ulaya. Kama utaamua kusafirisha kwa kutumia usafiri wa ndege hakikisha umefanya hesabu vizuri za bei ya kuuzia na utumie mawakala wanaotambulika kisheria kuepuka upotevu wa mzigo

C) Njia ambayo hutumika zaidi ulimwenguni Kote ni njia ya meli . Hii ni salama lakini huchukua muda . Ukitumia mawakala ( clearing and forwarding agents) husika ni kazi mzigo wako kupotea

7. Mabadiko ya uhitaji ( Change in consumers preferences/ consumers dynamism)

Uhitaji wa mazao ya kilimo habadilika kulingana na misimu, uhitaji na uwezo wahitaji. Mfano ni kazi sana kuuza matikiti maji kipindi cha mvua  . Watumiaji wa nchi nyingine wana mitazamo tofauti , utumiaji tofauti na mfumo tofauti wa maisha. Hakikisha umeangalia misimu na umefikisha bidhaa yako sokoni kwa wakati . Ili kuendana na soko linachohitaji.



Hizi ni baadhi tu ya changamoto zipo nyingine nyingi .

Tunashukuru kwa kupitia makala hii . Ubarikiwe sana.

Na muandishi wako

Erick Muhini.

Wasiliana nasi kupitia

+ 255744207795

Post a Comment

0 Comments