1.Knowledge (Maarifa)
2. Experience (Uzoefu)
3. Connection(Rasilimali watu)
4. Blessings (Baraka)
Kila mwanadamu anatamani kutimiza ndoto zake kabla hajaondoka hapa duniani. Mafanikio yanaweza kuwa na maana tofauti kwa watu tofauti . Wengine mafanikio humaanisha kuwa na furaha ,wengine ni kumaliza taasisi fulani ya elimu , wengine nikumiliki kiasi fulani cha fedha , wengine ni kuwa na biashara kubwa , wengine ni kupandishwa cheo kazini na wengine ni kuwa na idadi kadhaa ya watoto . Kila mmoja humaanisha tofauti anapo sema mafanikio, kumbe mafanikio ni jambo binafsi kimaana na si swala la ujumla . Kuna mambo mengi mno ambayo yanamfanya mtu kupata mafanikio fulani kwenye eneo husika .Zifuatazo ni njia kuu nne zitakazo fanya uweze kuwa na mafanikio ama kama umeyapata basi yazidi kuwa makubwa zaidi . Njia hizi sio mpya pengine zote unazifahamu . Karibu twende pamoja katika makala hii.
1. MAARIFA ( Knowledge)
Nyuki hafundishwi kutengeneza asali ama samaki hafundishwi kuogelea . Lakini ili binadamu awe na maarifa ama ujuzi fulani ni lazima kujifunza kwanza.
Pengine umeshawahi kusikia toka maandiko matakatifu neno linasema , Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Maarifa ni chanzo cha kwanza kabisa kufanikiwa kwenye jambo lolote. Huwezi kuwa daktari mwenye mafanikio wakati hujajifunza udaktari. Kuna namna nyingi sana za kupata maarifa, moja wapo ikiwa ni shule . Njia nyingine ni kama ufuatiliaji kwa watu wanaofahamu kwa njia kama za mtandao ama kujifunza kwa kutazama waliofanikiwa kwenye jambo unalohitaji. Ni baada tu yakuwa na maarifa sahihi ndio unaweza kufanikiwa .Watu waliofanikiwa kwenye sekta unayo taka kufanikiwa kuna kitu wanakifahamu ambacho wewe bado hukifahamu . Hicho ndicho kinachokutofautisha wewe na wao . Tumia muda wako kujifunza kuwa mtu unae taka kuwa .
2. UZOEFU ( Experience )
Baada ya kupata maarifa yatakayo kujengea ujuzi na ufahamu katika sekta unayotaka kufanikiwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na uzoefu . Mtu mwenye uzoefu ni mtu alie na busara kubwa katika mahali alipo . Hii inamaanisha amekosea mara nyingi kiasi kwamba tayari anajua namna ya kupambana kipindi cha nyakati ngumu . Lakini mzoefu maana yake amejifunza kulingana na makosa na hapa ndipo swala la uvumilivu na kutokata tamaa huingia ndani . Mafanikio si swala la usiku mmoja ni safari ya kuanguka na kuinuka kisha kujifunza kulingana na makosa na kufanya kitu kwa usahihi zaidi. Mfano Thomas Edison mwanasayansi alie gundua taa za umeme alifanya majaribio zaidi ya mara 10,000 bila kukata tamaa ili kugundua taa za umeme tulizo nazo leo.
3.RASILIMALI WATU ( Connection)
Jiulize kitu kimoja ivi unadhani Ronaldo na Messi ndio wanaojua kucheza mpira vizuri dunia nzima ??? Pengine yupo ata mtu kijijini kwenu anajua mpira kuliko ata hao ila shida nani anamfahamu?? Changamoto.
Ivi huwa unajiuliza kama Harmonise asinge kutana na Diamond angekuwa na mafanikio kama aliyonayo leo? Pengine ndio ama hapana lakini swala la msingi hapa ni hili. Ili ufanikiwe lazima ukutane na watu sahihi kwa wakati sahihi. Takwimu zinasema tabia zako ama kipato chako ni wastani wa kipato cha watu watano unaotumia muda mwingi zaidi nao. Yani kama utatumia muda mwingi na wajinga wa 5 baada ya muda wewe utakuwa mjinga wa 6. Ama utatumia muda mwingi na watu 5 waliofanikiwa baada ya muda wewe utakuwa wa sita . Hii inaitwa " law of attraction " kumbe kama unataka kubadili tabia yako badili kwanza watu wanao kuzunguka . Ni watu wanao muinua mtu mwingine na ni watu wanao muangusha mtu mwingine.
4.Baraka ( blessings)
Binadamu ni kiumbe cha kiroho chenye mwili (we are spiritual being with bodies) tofauti na wanyama ambao ni viumbe vya kimwili vyenye roho. Pengine hapa tunaweza kubali kuwa kila mtu aliletwa duniani akiwa na kusudi (purpose) maalumu. Hapa ndio utakuta kuna watu ni walimu kumbe walitakiwa wawe wanajeshi. Kuna watu ni madaktari kumbe walitakiwa wawe wakandarasi . Huwezi kukutana na mkondo wa bahati ama baraka kama upo sehemu isiyo sahihi. Wengine wanaita " infinite intelligence " lakini swala hapa ni kwamba ili uwe na mafanikio sahihi, ya kudumu na yenye mwisho mzuri ni lazima utembee katika kusudi la Mungu. Yani uwe kwenye sehemu uliyotakiwa kuwa. " Ulipo moyo wako ndipo hazina yako ilipo" yaani unapenda kufanya nini ?? Na kitu utachokipenda utafanya kwa moyo wote na ubunifu wa hali ya juu . Hili litakusaidia ufanikiwe .
Nisindeleee kukuchosha sana ila haya ni baadhi tu katika mengi ambayo kama utayazingatia mafanikio litakuwa ni swala tu la muda . Kikubwa ni uvumilivu, kuomba Mungu na kufanya kazi kwa kujituma.
Asante sana kwa kusoma makala hii ubarikiwe sana .
Wasiliana nasi kupitia :
+ 255 744 207 795
Erick Muhini ( agro economists)
12 Comments
Blessings
ReplyDeleteMakala nzuri brother,endelea kutuelimisha,see you at the top 🔝
ReplyDeleteNilipoona notification chapu nimekimbilia nashukuru najengeka zaidi Naomba muwe mnatuwekea makala Mara kwa mara
ReplyDeleteendelea kufuatilia
DeleteAsante sana kwa kutufuatilia kumbuka kushare kwa wingi
DeleteHakika Mungu akubariki hii tovuti imekuwa darasa bora kwangu
ReplyDeletenimejifunza asante
ReplyDeleteasante sana endelea kufauatilia
DeleteMlitutupa sana ila tunashukuru kukumbukwa kwa makala hii adhimu yenye kujenga na kuelimisha
ReplyDeleteAsante sana uwe unatembelea kila wakati
DeleteMaandishi unastahili pongezi
ReplyDeleteAsante sana endelea kufatilia makala zetu
Delete