Leo tarehe 20 mwezi wa sita 2023 benki kuu ya Tanzania imetoa tamko linalo taka biashara nyingi zifanyike kwa shilingi . Je swala hili ni sawa kiuchumi ama si sawa, je litasaidia uchumi ama halitasaidia uchumi ? Hili linaenda sambamba kwa Benki kuu kuweka malengo ya kuanza kuihifadhi dhahabu . Je haya yote yana tija kwa uchumi wa taifa letu ama hayana.Ayaa twende kazi
Kama ilivyo ada turudi kidogo katika historia . Hivi umeshawahi kujiuliza kwanini tunatumia dola ya marekani kufanyia biashara kimataifa? Kwanini isiwe pesa nyingine? Ama kwanini biashara kati yetu na nchi jirani tu kama vile Kenya tunahitaji dola ya Marekani ?, Hili ni Swali aliuliza Rais wa Kenya.
Kama tulivyo jifunza katika makala ya nyuma, zamani watu walitumia dhahabu na vito vya thamani Kama njia ya kubadilishana . Nchi zilitengeneza fedha (fiat /paper money) kulingana na kiasi cha dhahabu zilizo kuwa nazo yanii kitalaamu (gold standard / currecy backed by gold) . Katika historia ya Dunia kuna baadhi ya pesa za nchi kadhaa zilishawahi kutumika kama pesa ya kibiashara ya dunia (world international currency). Mfano ni kama pesa ya Roma, pesa ya Ureno , pesa ya Uhispania na pesa ya Uingereza (great Britain pound). Je ni namna gani dola ya Marekani ilianza kutumika???
Kabla ya vita ya pili ya Dunia pesa ya Uingereza ndio ilitumika kama pesa ya dunia (global currency)
Hadi mnamo mwaka 1945 mwishoni mwa vita ya Dunia . Nchi zote zenye uchumi mkubwa zilikuwa zimeharibiwa sana na vita. Ni marekani pekee ndio nchi ambayo vita haikupiganiwa katika ardhi yake moja kwa moja . Na kwakuwa aliwauzia nchi nyingine silaha na hawakuwa na pesa yakumlipa alitaka wamlipe kwa dhahabu. Karibia mwishoni mwa vita kuu ya pili ya Dunia , Julai mwaka 1944 Marekani ilikuwa inamiliki theluthi mbili ya dhahabu ya Dunia.
Hali hii ilimpa uwezo wa kuweza kutengeneza (print) pesa nyingi zaidi. Lakini ilikuwa ndio nchi yenye nguvu kiuchumi na kiulinzi. Pia ilikuwa nchi yenye uwezo mkubwa wa kuuza bidhaa nje (exportation) sifa hizi zilifanya nchi nyingine kubwa 44 zikubaliane na kuingia mkataba (Bretton Woods Agreement) wa kutumia dola ya Marekani kwanza kama pesa ya biashara za kimataifa (international trade currency) lakini pia kama hifadhi ya benki kuu za nchi (global currency reserve). Hii inamaanisha ili fedha yako iwe imara (stable) ilikuhitaji kuwa na hifadhi ya dola ya Marekani katika benki yako.
Upo mpaka apo??
Yani kwa lugha nyepesi pesa ya marekani ilisapotiwa na dhahabu na pesa za nchi nyingine zilisapotiwa na pesa ya Marekani (American dollar was backed by gold and other world currency was backed by US dollar). Lakini pia Marekani iliingia mkataba na nchi ya Saudi Arabia (mzalishaji wa kwanza wa bidhaa za mafuta ya petroli) mkataba ulioitwa (Petrodollar Agreement) mwaka 1973. Mkataba huu ulifanya Saudi Arabia ikubali kuuza mafuta yake kwa dola tu na Marekani ikikubali kuipa ulinzi .Hii ilifanya nchi nyingine zote kuhitaji dola ili kuendesha uchumi wake kwa kuwa mafuta ni chanzo cha uzalishaji .
Je ni faida zipi ilipata nchi ya marekani
A) Iliweza kuwa na sauti kiuchumi na kiulinzi kwakuwa dunia nzima ilihitaji pesa yake.
B) Iliimarika kiuwekezaji kwakuwa mwisho wa siku watu waliwekeza hizo pesa Marekani . Mfano kwa sasa 40% ya uwekezaji wa soko la hisa la Marekani ni nchi nyingine kama Japani, China, Uingereza na nchi za Ulaya
C) Ilifanya pesa ya Marekani iwe na uhitaji mkubwa duniani kote
Mnamo mwaka 1971 Marekani ilikuwa na vita na nchi ya Vietnam. Katika muda huu Rais Nickson wa Marekani kipindi icho ,aliamua kusimamisha " gold standard " kwa muda kwakuwa kipindi hicho serikali ilihitaji pesa ili kupigana vita. Hii maana yake nini ?? Inamaanisha Serikali ya Marekani haikuweza tena kutengeneza pesa (money printing) kulingana na kiasi cha dhahabu kilichopo bali kwa matakwa ya serikali. Maana yake nini?. Pesa ya kimataifa tunayoitegemea inazalishwa kiholela tu kwa jinsi Serikali ya Marekani itakavyo jiskia . Kwanza hii ilikuwa kinyume na mkataba wa mwaka 1944. Kwa muda wa Karne mbili Benki kuu za Dunia zimepunguza hifadhi ya dola toka 78% hadi 58%.
Tutoke huko kidogo hii mada inahitaji muda kuiongelea turudi kwenye maswali yetu ya msingi.
JE BENKI KUU YA TANZANIA KUANZA KUHIFADHI DHAHABU KUNA TIJA KIUCHUMI???
Jibu ni NDIO ya herufi kubwa. Kwanza kama ulivyoona hapo mwanzo. Ili pesa iwe na thamani na iwe imara ni lazima ipigwe tafu na kitu halisi chenye thamani . Hapo mwanzo kitu hicho kilikuwa dola ya Marekani ila kulingana na kuanza kupungua kwa kasi , uhitaji na taswira ya Dunia kuhusu dola ya Marekani si Salama sana kwa nchi kuendelea kuhifadhi kitu kinachopungua thamani. Kwakuwa dhahabu imetumika karne na karne . Kwa benki kutumia dhahabu ku sapoti pesa yetu ni jambo la msingi sana kiuchumi . Hii itafanya pesa yetu kuwa yakuaminika zaidi katika siku za usoni . Na itasaidia kupunguza mfumuko wa bei kwakuwa kama pesa yetu itakuwa na nguvu kulinganisha na pesa zingine , Gharama za kuagiza bidhaa (importation cost) zitapungua na kufanya ghrama za uzalishaji kuwa ndogo hivyo kuzuia mfumuko wa bei (cost push inflation).
JE, KUPUNGUZA MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KWENYE BIASHARA ZA NDANI KUNA TIJA KIUCHUMI ???
Jibu ni NDIO kubwa . Kama kuna kitu Cha maana Gavana wa Benki kuu Mr. Tutuba amefanya ni hili swala .
Ili pesa yoyote iwe na nguvu kiuchumi ni lazima itumike . Kuna nchi ambazo hutumia pesa za kigeni hasa dola ya Marekani kama Zimbambwe na Congo DRC . Matokeo yake kiuchumi ni nini . Uhitaji wa pesa za kigeni unaongezeka (high demand) hii inasababisha thamani ya pesa hizo kuongezeka na ziliongezeka sababu ya uhitaji kwahiyo zinapunguza uthamani wa pesa yako (the higher the demand , the higher the price) . Yani kama pesa ya kigeni inaongezeka thamani kwako ,basi pesa yako inapungua thamani. Unapozidi kutumia pesa za kugeni ndani ya nchi unapunguza mzunguko wa pesa yako (velocity of money) na ukipunguza mzunguko wa pesa yako una punguza uthamani wako (purchasing power) Jambo hili linaweza pelekea mfumuko wa bei kwakuwa kuagiza bidhaa nje za uzalishaji ( Importation of industrial goods) itakuwa gharama na hili litapelekea mfumuko wa bei ( cost push inflation) . Mfumuko huo wa bei unaweza pelekea kudumaza uchumi kwakua utapunguza uhitaji wa bidhaa (decrese in public spending) na hili linapunguza pato la taifa kwa ujumla (negative economic growth)
Kwa ujumla maamuzi ya Benki kuu ni mazuri sana na yanatija kubwa kwa taifa letu.
Nashukuru kwa kupitia makala hii. Kama una swali ama maoni karibu.
Ubarikiwe sana.
Wasiliana nasi kupitia
+255744207795
BONYEZA HAPA kuwasiliana nami whatsapp
Erick Muhini (Agro Economist)
13 Comments
nimejifunza
ReplyDeleteAsante endelea kufuatilia makala zetu
Deleteupi mtazamo wako mwandishi umesimama mrengo gani
ReplyDeleteBinafsi naona kwa ulimwengu tulipo sasa ni vizuri sana kuimarisha kutumia pesa zetu zaidi .Hivyo benki kuu imefanya jambo la maana sana ,ila kuhusu upande ,sisi wowote tunasimama kwenye ukweli tu ,we are trained to read numbers
DeleteNi kweli kabisa tunapaswa kuwa positive kwa hili
ReplyDeleteendelea kufuatilia
DeleteMAKALA NZURI BANDO HALIJAENDA BURE KUSOMA
ReplyDeleteasante share zaidi kwa ndugu na marafiki
DeleteAmbao hatujui dola ni nini na matumizi yake koment zetu tunaweka wapi
ReplyDeletehapa ili tukusaidie
DeleteHAMNA KUNDI LA WHATSAPP AGRO OTTOMANS
ReplyDeleteBado hatujafungua kaka ila uki bofya alama ya what's app unawasiliana nasi moja kwa moja mkuu
Deletemmesikia dola imepanda huko 2800
ReplyDelete