Ticker

6/recent/ticker-posts

MAMBO MAKUU MATANO YAKUNZINGATIA KABLA HUJAWEKA PESA YAKO KWENYE UWEKEZAJI WA KILIMO

1. Taarifa sahihi

Hakikisha una taarifa sahihi katika aina ya uwekezaji unaotaka kufanya . Taarifa sahihi hutegemea aina ya mtu ama watu waliokupa taarifa hizo . Anae kupa taarifa itafaa sana kama ni mtu ambaye aidha amewahi fanya uwekezaji huo ama utafiti wa kutosha kwa uwekezaji husika .Taarifa sahihi ndio chanzo cha kufanya biashara yako isimame . Katika kilimo huwa tunatumia bei za msim uliopita kujaribu kuangalia bei za msim ujao yaani kitaalam ( Cobweb Model) . Hii ni njia sahihi lakini inabid kulinganisha miaka kadhaa ya nyuma ya tabia za masoko, bei na mifumo ya serikali ili kuweza kufanya maaamuzi sahihi . Njia hii kitaalamu inaitwa (Trend analysis)

                       

2. Mtaji

Mtaji si lazima uwe wa fedha . Unaweza kuwa na mtaji wa fedha, watu , ardhi, taarifa ama mawazo. Kulingana na sehemu ya mnyororo wa thamani unaotaka kuwekeza yani mathalani shambani, sokoni , usafirishaji ama uchakataji . Hakikisha una aina ya mtaji unaoitajika. Kama unahitaji kuwekeza kwenye masoko hakikisha una mtaji mkubwa wa taarifa za masoko. Kama unapenda kuwekeza kwenye kutoa huduma Kama semina, hakikisha una mtaji wa kutosha wa mawazo . Mfano kwa mtu anae taka kuwekeza shambani lazima awe na mtaji wa fedha, ardhi , watu  na kadhalika . Ieleweke kuwa mtaji katika uwekezaji si fedha peke yake . Na wakati meingine unaweza kuwekeza bila kutumia fedha ( skills investment ). Ukubwa wa mtaji utasaidia mambo kadhaa.

a) ukubwa wa biashara utakayo ifanya

b) kiasi cha ukuwaji wa biashara yako

c) Jinsi unaweza kusimama pindi biashara yako imeanguka

d) Ukubwa ama udogo wa biashara yako na uwezo wa kupambana na misukosuko

Uwekezaji katika kilimo hasa shambaani unahitaji mtaji wa kutosha . Hakikisha kiwango cha uwekezaji ( scale of investment) inaendana na mtaji na muda ulionao.

3. Maarifa ( elimu)

Warren Buffet muwekezaji mkubwa ( investor of all time )zaidi duniani aliwahi kusema  ivi " kama haujui kila kitu kuhusu biashara yako lazima biashara hiyo itakufa ". Wengi wanadhani ukishakuwa na mtaji tu unaweza kuwekeza kwenye kilimo. Kilimo ni uwekezaji ambao ni rahisi sana kupoteza mtaji wako wote . Hili linatokana na kuwa kilimo ni uwekezaji ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea uhitaji na ugavi ( forces of supply and demand) . Kiuchumi kilimo hufananishwa na biashara huria ( perfect competitive market ). Swala hili hufanya bei za bidhaa za kilimo kubadilika mara kwa mara . Na kwakuwa kilimo hutegemea sana mabadiliko ya tabia ya nchi , uwekezaji huu unaitaji sana maarifa na elimu ya kutosha . Unaweza pata elimu hii kwa kujifunza katika semina na makala mbalimbali . Tumia muda mwingi kujifunza kabla haujaanza kufanya uwekezaji katika kilimo. Wengi wamekuwa wakikurupuka  na wakijikuta wanapoteza pesa nyingi .

4. Uwezo

Ifahamike kwamba si kila mtu anaweza kuwa muwekezaji na si kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara. Uwekezaji wa aina yoyote unahitaji uwezo wa kifikra, kimtazamo , kitabia na kimatendo .
Hakuna uwekezaji ama biashara ya aina yoyote isiyo na misukosuko . Hasa katika kilimo . Kuna siku utatumia milioni ishirini kulima alafu ikanyesha mvua kubwa siku moja na mazao yote yakaharibika  . Utakapo amua kuwekeza katika kilimo hakikisha una mtazamo sahihi kuhusu kilimo na uwekezaji. Uwe na moyo wa uvumilivu sababu uwekezaji katika kilimo unachukua muda .Uwekezaji wa kilomo sio wa kupata pesa usiku moja ( quick get rich scheme) . Unahitaji ufanisi , uvumilivu na mtazamo chanya siku zote ili kuweza kuanza kupata mrejesho sahihi ( positive return) . Kama hauna uwezo wa kuvumilia hasara , kuvumilia kupoteza kuwekeza kwa miaka kadhaa ili unufaike badae basi sekta ya kilimo sio sahihi kwako . Chukulia mfano wa mtu anae panda miti anavumilia pengine hadi miaka  thelathini ndio aanze kuvuna . Kwa miaka io thelathini anawekeza  pesa, muda, watu na ujuzi . Ili aje apate badae . Sio kila uwekezaji utahitaji muda huu. Ila la msingi zaidi ni kuwa na utayari wa kukubali kuwekeza muda, pesa , ujuzi na maarifa leo ili uje upate badae .

5.  Chagua eneo la kuwekeza

Sekta ya kilimo ni pana sana . Katika mnyororo wa thamani wa kilimo kuna sehemu kama shambani, sokoni, usafirishaji , kuchakata ama kuongeza thamani.
Shambani kuna fursa nyingi kama mbegu, udongo, chakula cha mifugo,mashine na mazao tofauti tofauti.
Sokoni kuna fursa kama kutafuta masoko, kuwa na taarifa za masoko ama kuunganisha wakulima na masoko, ama kutangaza mazao ya kilimo mtandaoni  yaani ( Agricultural digital marketing)
Usafirishaji una fursa katika kutoa mazao sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa kuwa sekta ya kilimo ni pana ni kazi kubwa  kuwekeza katika kila myororo wa thamani . Itambidi muwekezaji kuchagua wapi atawekeza . Na kama atamua kuwekeza katika mnyororo wote wa thamani ( vertical integration) basi itamlazimu muwekezaji achague mazao kadhaa ya kufanya hivi . Uwekezaji wa namna hii utahitaji pesa, muda na rasilimali watu na ardhi yakutosha kama utakuwa mkubwa.
Ili uweze fanikiwa katika uwekezaji wako wa kilimo ni vema ukachagua sehemu maalum  ( specific value chain node) ili uwekeze muda wako apo ujifunze zaidi ,utengeneze uwezo wako hapo kisha uwekeze katika eneo hilo . Uwekezaji katika kilimo utafaida na tija  kubwa sana . Hasa katika taifa letu lenye vijana, tabia ya nchi inayoeleweka  na ardhi ya kutosha . Kwakua tunataraji ongezeko kubwa la watu uhitaji wa chakula unaongezeka kila leo . Hili linafanya kilimo kuwa biashara kubwa na sahihi katika siku za usoni.
                 

Tunashukuru  kwa kupitia makala hii ubarikiwe usiache kufuatilia tovuti yetu kila siku

Ni muandishi wako
Erick Muhini ( Agro Economist )
Wasiliana nasi 
+255744207795



Post a Comment

0 Comments